Proffesor Jay Asema "Tumechoka kuzika nguo", Serikali Yamjibu

Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Proffesor Jay) jana  alisema kuwa zaidi wananchi 40 wa  kata ya Luhembe, Jimbo la Mikumi wamepotea na hawapatikani.

Mbunge huyo alihoji Serikali ina sema nini juu ya wananchi hao wanaopotea na hawaonekani na tabia ya watumishi wa TANAPA kuwachukua wakazi wa Mikumi na kuwatesa.?

Akijibu swali hilo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alimuagiza ‘Prof. Jay’, kupeleka ushahidi wa madai yake ili serikali iyafanyie kazi.

Hasunga alisema; "Mheshimiwa Mbunge naomba ulete ushahidi wa kupotea kwa wananchi ili kutanabaisha taarifa hizo na serikali itashughulikia suala hilo maana serikali ipo kwa kulinda usalama wa wananchi”.

Naibu Waziri aliongeza kuwa serikali tayari imetatua mgogoro wa mpaka kati ya wakazi wa Mikumi na maeneo ya hifadhi.


from MPEKUZI

Comments