Pikipiki na Magari ya mashindano nazo kuondolewa kodi

Waziri wa Fedha, Philip Mpango amesema serikali inatarajia kufanya mabadiliko kwenye sheria ya forodha la jumuiya ya Afrika Mashariki inayotoa msamaha wa kodi kwa magari yanayotumika kwenye mashindano ya mbio za magari na kujumuisha pikipiki kwenye msamaha huo.

Waziri Mpango ameyasema hayo leo Juni 14 wakati akiwasilisha bajeti kuu kwa mwaka wa fedha, 2018/19, bungeni.

 “Hatua hiyo inatarajiwa kuhamasisha mashindano hayo na kukuza sekta ya utalii nchini,” amesema

Dk Mpango pia amesema serikali imepanga kuondoa tozo kwa vifaa vya zima moto, tozo ya ushauri kuhusu usalama wa afya.

Amesema hatua za upunguzaji wa kodi na tozo, zitaanza kutekelezwa Julai mosi, mwaka huu.


from MPEKUZI

Comments