Moto Waua Watu 15 Nchini Kenya

Takriban watu 15 wamefariki katika moto mkubwa uliokumba soko moja katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Zaidi ya watu 50 wamejeruhiwa katika moto huo uliotokea usiku wa leo  na kusababisha uhuribifu wa mali nyingi.

Soko hilo la Gikomba ndio soko kubwa zaidi katika mji huo na moto hutokea mara kwa mara swala linalosababisha uvumi kwamba huenda kuna watu wanaochoma soko hilo.

Jeshi la Polisi nchini humo limesema kuwa bado linafanya uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo ulioteketeza mali nyingi za Wafanyabiashara katitka soko hilo na kuunguza baadhi ya nyumba zilizopo jirani na soko hilo.


from MPEKUZI

Comments