Kipa wa Iceland aibuka mchezaji bora

Golikipa wa timu ya taifa ya Iceland, Hannes Þór Halldórsson, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika mchezo wa leo dhidi ya Argentina kwenye michuano ya Kombe la Dunia.

Halldorsson amepata tuzo hiyo baada ya kuokoa mipira mingi ya wachezaji wa Argentina ikiwemo penati ya Lionel Messi, ambayo ilionekana kumaliza furaha ya mchezaji huyo uwanjani.

Katika mchezo huo, mechi hiyo imeweza kumalizika kwa matokeo ya 1-1 na timu zote kuweza kuambulia alama moja.

Kipa huyo amemzuia Messi kujibu mapigo ya Hat-Trick aliyoyafanya Ronaldo jana dhidi ya Spain, Iceland imekuwa taifa dogo zaidi kushiriki kwenye michuano ya Kombe la dunia.


from MPEKUZI

Comments