Kamati ya Bunge ya Bajeti imeishauri Serikali kutofuta kifungu cha 17A cha Sheria ya Sekta ya Korosho ili kuruhusu ushuru unaotokana na mauzo ya korosho ghafi nje ya nchi kuingizwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
Kamati hiyo imesema asilimia 65 ya ushuru wa Korosho unapaswa kuachwa ili fedha hizo zipelekwe katika mfuko wa bodi ya korosho kupitia Wizara ya Kilimo.
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Juni 28, 2018 bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Ghasia.
“Kwa kuwa majukumu ya kuendeleza zao hilo yamehamishiwa Bodi ya korosho, fedha zipelekwe bodi ya korosho kupitia wizara ya kilimo,” amesema Ghasia ambaye pia ni Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM).
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment