Gambo awaomba BAKWATA kupiga marufuku Waumini Kucheza Kareti Misikitini

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amelitaka Baraza Kuu la Waislamu mkoani Arusha kukemea tabia ya baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu kucheza mchezo wa kareti misikitini na kusisitiza kwamba tabia hizo haifai.

Gambo ametoa kauli hiyo jana, Juni 15 mara baada ya ibada ya sikukuu ya Eid iliyofanyika katika uwanja wa  Sheikh Amri Abeid jana  mkoani Arusha na kuwataka Bakwata kukemea tabia hiyo.

Mh. Gambo amesema kwamba tabia ya baadhi ya misikiti kufundisha waumini wake mchezo wa kareti ndani ya misikiti haifai na inapaswa kukemewa.

“Baadhi ya misikiti kufundisha karate haifai naomba niwapongeze Bakwata kwa kukemea tabia hii na ninawaomba muendelee kulisimamia hili” amesema Gambo


from MPEKUZI

Comments