Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Chande maarufu kama 'Dogo Janja' ambaye pia ni mume wa msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amedai katika ndoa yao yeye ndio mwanaume na mwenye sauti ya kutoa maamuzi ya jambo lolote tofauti na watu wanavyomfikilia.
Dogo Janja amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na kituo cha EATV baada ya kuwepo kwa tetesi za kipindi kirefu zilizokuwa zinadai Janjaroo hana maamuzi yoyote katika ndoa yake kwa kuwa mwenye sauti ya kuamua jambo lolote ni mke wake Irene Uwoya.
"Ukiwa hauna maamuzi au sauti kwa mke wako wa halali ni kitu kizuri sana tofauti ukiwa hauna sauti kwa hawala. Mimi nina mtii mke wangu naye pia anafanya hivyo, kwenye ndoa yangu nina simama kama baba", amesema Dogo Janja na kuongeza;
"Watu wengi wanachukulia mambo kwa juu juu tu kwa mzaha, mimi nina sauti kwa mke wangu ninaweza kumwambia leo usitoke na huwa atoki au asifanye kitu fulani na akanisikiliza, 'so' sio kila jambo nitakalo mkataza basi nitangaze ila mpaka mke wangu akifanya jambo fulani mjue nina taarifa nayo na ninaelewa. Ndoa ni taasisi kubwa sana tofauti na watu ambao wapo tu mtaani wanatoa maamuzi yao bila ya kuelewa".
Kwa upande mwingine, Dogo Janja amedai watu wengi wamekuwa wanaongelea kuhusiana na ndoa yake kwenye mitandao ya kijamii bila ya kuwa na ufahamu wa aina yoyote juu ya taasisi hiyo ambayo ina uwanja mpana ndani yake.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment