Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Banana’ Dogo Janja amedai msanii kutoka label ya WCB Rayvanny anamuangusha sana Kwenye suala la mavazi.
Siku za nyuma Dogo Janja ameshawahi kuachia ngoma maalumu kwa ajili kuvaa na kupendeza Inayoitwa ‘Ukivaaje unapendeza”.
Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kama akipata fursa ya kumvalisha Rayvanny atafanya hivyo.
"Nikiambiwa msanii ambaye niwe namvalisha namchagulia mavazi, nitamchagua Rayvanny huwa ananiangusha sana sometimes.
"Kuna muda huwa anapatia halafu kuna muda unaweza ukatema mate kule, anaweza akala njano juu mpaka chini”.
Dogo Janja yupo katika Media Tour kwa ajili ya kutangaza rasmi Single yake mpya ‘Banana’ inayoendelea kufanya vizuri Kwenye chati mbali mbali.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment