Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete ametoa pongezi zake za dhati kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM aliyeomba kujiuzulu nafasi hiyo mara baada ya kutumikia kwa muda mrefu, Abdulrahman Kinana.
JK amemshukuru Kinana kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya kipindi chote alichotumikia nafasi hiyo katika Chama Cha Mapinduzi CCM na kumtakia kila la kheri katika safari yake ya maisha ya kustaafu.
Aidha ametumia nafasi hiyo kumkaribisha mteuliwa mpya wa nafasi hiyo, Dk. Bashiriu Kakurwa na kumpongeza kwa kuaminika na Serikali nzima ya CCM na kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na kuwa Katibu Mkuu wa CCM.
Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete alitumia ukurasa wake wa Twitter kutoa pongezi hizo za dhati kwa viongozi hao ambapo ameandika hivi.
“Kwa heri Kinana. Hongera kwa kazi nzuri. Daima tutakukumbuka. Hongera Bashiru. Nakutakia kila la heri. Hongera @ccm_tanzania , hongera Mwenyekiti @MagufuliJP Umoja ni Ushindi, Kidumu Chama Cha Mapinduzi !”
Aidha, amempongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kwa kukiendesha vyema chama hicho huku akiwataka wanachama wake waendeleze umoja wao.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment