Na. Dokta Mungwa Kabili…..0744 000 473.
Jina halisi la mti huu ni MKUNGA-NYOTA na sio MGUNGA –NYOTA kama baadhi ya watu wanavyo uita kimakosa.
Unaitwa Mkunga –Nyota kwa sababu ya kuwa na sifa kuu mbili za kipekee ambazo ni kwanza ni kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutibu tatizo la kutobeba ujauzito lakini pili kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuondosha nuksi na mikosi na kupandisha nyota.
Wengine wana uita Mkunga-Marashi kwa sababu ya kuwa na sifa ya kutoa harufu nzuri sana pindi unapochemshwa kwenye maji na kutoa moshi unao nukia vizuri pindi unapo unguzwa au kuchomwa moto.
Vile vile mti huu hujulikana kwa wengine kama UZAZI WA KARIBU kwa sababu ya kutumiwa sana na wanawake wanao taka kuzaa kwa karibu karibu.
Ni mti wenye msaada mkubwa sana kwa wanawake wenye kusumbuliwa na tatizo la kutokubeba ujauzito.
Kama wewe ni mwanamke ambae unasumbuliwa na tatizo la kutoshika ujauzito na umehangaika kutumia tiba mbalimbali kwa muda mrefu bila mafanikio basi nakushauri ujaribu kutumia tiba ya mti huu na Inshaalah utabeba ujauzito bila wasi wasi wowote.
Katibu kutibu tatizo la kutobeba ujauzito , mti wa Mkunga Nyota una msaada mkubwa sana katika kufungua na kusafisha njia ya kizazi pamoja na kurutubisha mayai ya uzazi.
Wakunga wa jadi katika maeneo mbalimbali vijijini wanautumia mti wa Mkunga-Nyota kuwakinga wanawake wajawazito dhidi ya tatizo la kushikwa na uchungu kwa muda mrefu pamoja na kuzuia tatizo la kiunga mwana kutoka nje kabla mtoto hajazaliwa wakati wa kujifungua.
Vile vile wakunga wa jadi huutumia mti wa Mkunga – Nyota kuwakinga wanawake wajawazito dhidi ya tatizo la mtoto kulalia upande katikati ya njia ya kizazi bila kukaa wima jambo ambalo haliwezi kuruhusu mtoto kuzaliwa kwa njia ya kawaida na hivyo kuondosha ulazima wa mwanamke kujifungua kwa njia ya operesheni.
Mti wa Mkunga –Nyota pia ni msaada mkubwa sana kwa wanawake wenye tatizo la kutokwa na uvimbe wa tumboni ( fibroid ). Mti huu huyeyusha na kuondosha kabisa uvimbe wa tumboni bila kujalisha uvimbe huo ni mkubwa kwa kiasi gani .
Katika kuyeyusha uvimbe wa tumboni mti wa Mkunga - Nyota unafanya kazi kwa ufanisi mkubwa kuliko mizizi ya mpamba pori ambayo imekuwa ikitumiwa na wengi katika kujitibu tatizo la kutokwa na uvimbe tumboni.
Mizizi ya mpamba pori huyeyusha fibroid kwa muda tu na badae uvimbe huo hurudi tena kwa kasi ya ajabu na kusababisha mgonjwa kulazimika kutumia tena dawa na hivyo kufanya maisha yake yote yawe ni ya kutumia dawa kila baada ya kipindi Fulani.
Mti wa Mkunga Nyota unaondoa uvimbe wa tumboni moja kwa moja . Uvimbe ukisha yeyuka basi haurudi tena.
Vile vile mti wa Mkunga Nyota hutoa msaada mkubwa sana kwa wanawake wenye tatizo la kuchoropokwa mimba .
Kama wewe ni mwanamke ambae umekuwa ukisumbuliwa na tatizo la kuchoropoka mimba na umejaribu kutumia tiba nyingi kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote maana yake ni kwamba haujawahi kutumia mti wa Mkunga Nyota kwa sababu mti wa Mkunga Nyota hutibu na kuondosha kabisa tatizo la mimba kutoka kabla ya wakati wake.
Hata wale wanao tumia zindiko la nge katika kujikinga na tatizo la kuchoropoka mimba huwa wanatumia mti huu wa Mkunga Nyota pamoja na nge.
Huwa anachukuliwa nge jike anaunguzwa pamoja na mti wa Mkunga Nyota hadi vyote viwe majivu halafu mwanamke aliye beba mimba ana chanjwa na kupakwa kiuoni kulia na kushoto, basi ujauzito hauwezi kuchoropoka hata kama alitegwa kwa uchawi wa kinyonga.
Labda kwa ufafanuzi hapo, nge ni miongoni mwa viumbe wachache wa Mwenyezi Mungu ambao wamepewa karama ya kutosumbuliwa na tatizo la mimba kutoka .
Nge akibeba ujauzito ni lazima azae . Mimba haiwezi kutoka kwa namna yoyote ile wala hawezi kupatwa na tatizo lolote lile wakati wa kuzaa.
Nguvu hii ya kiroho ya nge ndio inayo unganishwa na nguvu ya kiroho ya mti wa Mkunga Nyota kumkinga mwanamke aliye beba ujauzito usichoropoke.
Uchawi huu husimamishwa kwa damu ya kasuku au kunguru kwa sababu hao ndio wanyama ambao damu zao hutumika kama lango la kuunganisha nguvu kati ya wanadamu na wanyama.
Uchawi wa kinyonga kwa wajawazito hutumika ili kutengeneza umauti na matatizo kwa mwanamke mjamzito wakati wa kujifungua.
Huwa inanuiziwa afe mama wakati wa kujifuungua au wafe wote mama na mtoto . Mtoto anaweza kupona lakini mama huwa ni lazima afe.
Kutengeneza uchawi huo wachawi humchukua kinyonga aliye pasuka tumbo na kufa baada ya kuzaa . ( Kwa wasio jua , kuna aina ya vinyonga ambao hupasuka tumbo na kufa wakati wa kujifunga. Vinyonga hawa huwa hawakutani na watoto wao. .Vinyonga hawa hubadilishana kifo kwa uhai wa watoto wao )
Pia hutafutwa kondoo mjamzito halafu huchinjwa na kupasuliwa tumbo kisha mtoto wa kondoo alie tumboni ambae bado anakuwa anapumua wakati huo huuwawa kwa kisu na baadae hukaushwa na kuchanganywa na madawa mengine ya kichawi pamoja na Yule kinyonga halafu uchawi huo unaenda kutegwa kwenye njia anayo tumia kupita mwanamke alie kusudiwa au kama yupo mbali hutegwa njia panda nne na kutumwa kwa mhusika.
Basi mhusika lazima atakufa wakati wa kujifungua .
Mti huu wenye maajabu hutumika pamoja na yai la kuku wa kienyeji katika kujua kama mwanamke mjamzito atajifungua salama au atajifungua kwa matatizo na kama ikionekana kuwa mwanamke huyo ata jifungua kwa matatizo basi mti hutumika kubatilisha matatizo hayo.
Kinacho fanyika unachukuliwa mti wa Mkunga Nyota na kusagwa upatikane unga wake kisha unachanganywa na zaafarani ya njano , asali kijiko kimoja na mafuta ya zeituni kijiko kimoja, halafu linachukuliwa yai jeupe la kuku wa kienyeji, linafanyiwa duwa maalumu na kuchorwa alama maalumu kwa juu kwa kutumia unga wa mti wa Mkunga Nyota ulio changanywa na zaafarani ya unga ya rangi ya njano, asali na mafuta ya zeituni, kisha yai hilo linawekwa na kuzungushwa tumboni mwa mwanamke mjamzito kwa dua maalamu halafu baadae linapasuliwa kwenye chungu au kigae kilichotumika na kila kita onekana ndani ya chungu hicho.
Yai likiwa jeupe na ute wa njano basi ni ishara kuwa mwanamke huyo atajifungua salama salimini bila tatizo lolote.
Ikitokea alama ya damu kama ni alama moja kama vile kidoa kimoja au kimstari kimoja basi eidha mama au mtoto atafariki wakati wa kuifungua, vikitokea viwili basi mama na mtoto wote watafariki.
Ishara ni nyingi sana na tafsiri zake ni nyingi sana. Kwa kutumia mti huu huu na yai unaweza kugundua jinsia ya mtoto au kama ni mapacha watoto watakao zaliwa.
Kama nilivyo tangulia kusema hapo juu kuwa mti huu pia hutumika katika kuondosha mikosi na kupandisha nyota.
Na katika kupandisha nyota mti unatajwa kama miti iliyo katika daraja la juu kabisa na wenye uwezo mkubwa sana wa kuondosha nuksi, mikosi na kupandisha nyota.
Katika kupandisha nyota mti huu unatumika kwa kuogea , kuchanja, kupaka au kufukiza.
Vile vile mti huu unaingia kwenye nyungu za aina zote. Kuanzia nyunga ya mti mmoja, nyungu ya miti 7, nyungu ya miti 12, nyungu ya miti 40, hadi nyungu ya miti 77.
Katika makala zangu zijazo nitaelezea kuhusu namna mti wa Mkunga Nyota unavyo tumika katika kuondosha mikosi mwilini na kupandisha nyota.
MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI. ANAPATIKANA KWA SIMU NAMBA : 0744 000 473. BLOGU: https://ift.tt/2JaP3KM
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment