Mbunge CHADEMA Afariki Dunia

Mbunge wa jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma kupitia CHADEMA, Mh. Kasuku Samson Bilago amefariki dunia leo mchana akiwa katika Hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe.

Kuhusu chanzo cha kifo chake, Mbowe amesema:"Kwa sasa si wakati wake, tunahangaika kuhamisha mwili kutoka wodini kwenda chumba cha kuhifadhia maiti.  Hayo mengine itakuwa baadae."

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Habari wa chama hicho, Tumaini Makene amesema taarifa zaidi zitatolewa baadaye na chama hicho.

Bilago alishiriki baadhi ya vikao vya Bunge la bajeti lililoanza Aprili 3, 2018 mjini Dodoma.

Mheshimiwa Bilago pia alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA.


from MPEKUZI

Comments