Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Yatoa Ushauri Mzito Kwa Serikali

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, imeitaka serikali isiwe inatenga bajeti kubwa za wizara wakati haina uwezo wa kupeleka katika wizara fedha zote zinazopitishwa na bunge.

Ushauri huo ulitolewa bungeni jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nape Nnauye alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati yake baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangallah kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Hoja ya nape ilikuja baada ya kuona bajeti ya wizara hiyo imepungua kwa asilimia 22.1 ikilinganishwa na bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka uliopita.

“Kutokana na kasoro hiyo, kuna uwezekano kwa baadhi ya miradi ya wizara hii kutotekelezwa kutokana na uhaba wa fedha.

“Kamati inaishauri serikali isitishe zoezi la uwekaji wa vigingi vya mipaka katika mipaka ya hifadhi ili kuondoa malalamiko yaliyopo miongoni mwa wananchi wanaoishi jirani na maeneo hayo ya hifadhi,” amesema Nape.


from MPEKUZI

Comments