Inasemekana Tecno Kuja Na Tecno Spark KivIngine.

Kwa mara nyingine tena inasemekana kampuni ya simu ya TECNO ipo mbioni kuachia simu mpya ikidhaniwa kuwa ni muendelezo wa toleo la spark. Tetesi zimekua zikizagaa kwa wingi zaidi hasa mitandaoni na inasemekana simu hiyo itaingia sokoni tarehe 14/6/2018.
 
Na kulingana na vuta nikuvute za kuhusiana na jina la simu pamoja na sifa zake wadau wameamua kuipachika jina la utani kama TECNO SPARK 2, kwani toleo la spark ni moja kati ya matoleo ya TECNO yenye ushawishi mkubwa sana hasa ukizingatia ubora wake wa kamera pamoja na maumbo ya kuvutia. 
 
Hivyo basi inasemekana TECNO SPARK 2 ni zaidi ya spark yoyote maana safari hii inategemewa kuja kivingine ikiwa imeboreshwa zaidi kwa mfumo wa android. SPARK 2 inasemekana kutumia mtandao wenye kasi zaidi ya ule wa 4G eti wanasema ukigusa tu umenasa.

Hadithi za kuhusiana na simu inayosemekana ni TECNO SPARK 2 hazikuishia hapo kwani inasemekana eneo kubwa la TECNO SPARK 2 lenye nchi kama 6.0 HD+ au zaidi ni kioo kitupu chenye kuifanya simu kuwa na mvuto zaidi.  
  
Na mvutano unaonekana kuwa mkubwa zaidi katika upande wa ‘security’ kuna wanaosema iwe isiwe lazima TECNO SPARK 2 itakuwa na ‘security’ zaidi ya moja na moja wapo ikiwa ni FACE ID na nyingine haijatambulika maana wadau wanadai SPARK 2 kuwa simu ya kwanza na aina hiyo ya ‘security’.
Tetesi zinadai TECNO SPARK 2 itakuwa na aina mpya ya kionjo kwenye kamera ‘MIX FLASH’ ambacho hupiga picha yenye kung’aa mithili ya kioo na inasemekana ufanyaji wake kazi ni kama flashi 3 au zaidi ya tatu. 

Na endapo hizi tetesi zikawa na ukweli haswa kuhusiana na hiyo MIX FLASHI ni ngumu kutabiri itakuwa na picha nzuri kiasi gani kwani inasemekana  SPARK 2 inapixel za kamera 13+8 au zaidi.


from MPEKUZI

Comments