Dr. Helen Kijo-Bisimba Ang'atika LHRC....Bi. Anna Henga Achukua Mikoba Yake

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) imemtangaza Bi. Anna Henga kuwa Mkurugenzi mpya wa kituo hicho ambapo atapokea mikoba ya Mkurugenzi wake wa muda mrefu, Dr. Helen Kijo-Bisimba.

Uteuzi wa Bi. Henga ni matokeo ya mchakato wa ndani wa muda mrefu uliotekelezwa na bodi ya Wakurugenzi ya kituo hicho kutoka mwanzoni mwa mwaka 2017.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Kituo hicho imeeleaa kuwa uteuzi wa Bi. Henga unatarajiwa kuanza Julai 1 mwaka huu..

Awali Bi. Henga alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu


from MPEKUZI

Comments