Serikali Imewataka Wadau Wa Uwekezaji Kuacha Kulalamika Na Badala Yake Watoe Ushauri

NA Mahmoud Ahmad, DODOMA
SERIKALI imewataka wawekezaji na wadau mbalimbali kuachana na tabia ya kulalamika serikali na badala yake watoe ushauri kwa serikali ni jinsi gani ya kutatua changamoto mbalimbali.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Biashara Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage.

Mijage alitoa kauli hiyo jana wakati  alipokuwa akifungua mkutano wa wadau na wawekezaji wa pamba,bidhaa za nguo na mavazi katika ukumbi wa mikutano wa Hazina mjini hapa.

Alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazokabiliana na wizara hiyo lakini ni wakati wa wadau kutoa maoni yao ya kuishauri serikali pamoja na kuisaidia ili iweze kufanikiwa badala ya kuendelea kulalamika.

Hata hivyo alisema kwa kuzingatia kuwepo kwa sera ya serikali ya viwanda ni wakati sasa wa waekezaji kujenga viwanda ambavyo vitaweza kuzalisha malighafi ambazo zinazalishwa nchii badala ya kuuza malghafi hizo nje na kununua bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.

Akizungumzia zao la pamba alisema kwa kuwa wananchi na wakulima wamehamasishwa zaidi kulima pamba katika maeneo ya ukanda wa pamba ni lazima pamba inayozalishwa nchini isiuzwe nje ya nchi na badala yake ichakatwe na kuzalisha nguo na nyuzi ambazo zinaweza kutumiwa na kuzalisha bidhaa bora.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro,Siriel Mchembe,  ameitaka serikali kuhakikisha inaweka mikakati ambayo inaeleweka kwa lengo la kujua soko la pamba pamoja na bei ambayo itakuwa inamanufaa kwa wakulima.

Akichangia katika mkutano huo mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa amemwakilisha mkoa wa Morogoro, alisema kwa sasa wananchi wamehamasishwa zaidi kulima zao la pamba na kufikia hatua ya kuachana na kilimo cha mahindi hivyo wanatakiwa kuhakikishiwa kama pamba yao itakuwa na soko la uhakika.

“Kwa sasa wakulima wamehamasishwa sana kulima pamba imefikia hatua wapo wakulima ambao wameachana na kulima mahindi wakijua kuwa pamba itakuwa na bei nzuri, sasa ikitokea pamba ikaa haina soko au kuonekna ni chafu je wakulima hao tutawaambia nini” alihoji mkuu huyo wa wilaya.

Naye mkuu wa mkoa wa Mara Adam Kigoma Malima alisema haiweze, Mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya pamoja na wetendaji wengine wakaishi kwa kulalamika badala ya kutafuta suluhusho.

Alisema suala la uwepo wa viwanda unatakiwa kuwa na mikakati ya pamoja nadala ya kuishi kwa malalamiko na kukosa ufumbuzi na maazimio ya pamoja na kwa hali hiyo haiwezekani pakawepo na maendeleo.


from MPEKUZI

Comments