Ripoti ya CAG yaondoka na meneja kitengo cha bahari

Meneja kitengo cha bahari na maeneo tengefu, Dk Milali Machumu amesimamishwa kazi ikielezwa kuwa ameshindwa kukisimamia ipasavyo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema mbali na kumsimamisha kazi, amevunja bodi ya wadhamini ya kitengo hicho na ameagiza Dk Machumu achunguzwe.

Mpina amesema hayo leo Jumatatu Aprili 16, 2018 alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma akitoa ufafanuzi wa kasoro zilizoainishwa katika taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2016/17 zinazohusu wizara hiyo.

 “Kwa mamlaka niliyonayo kulingana na sheria ya kitengo cha hifadhi za bahari na maeneo tengefu, Namba 29 ya mwaka 1994 nanatoa maelekezo yafuatayo
  1.  Namsimamisha kazi Meneja wa kitengo cha bahari na maeneo tengefu (MPRU) Dr Milali Machumu mara moja kwa kushindwa kusimamia ipasavyo kitengo hiki, pamoja na kumsimamisha kazi pia atachunguzwa
  2.  Ninavunja Bodi ya wadhamimi mara moja na kuisuka upya
  3.  Ninamwagiza Katibu mkuu wa Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuunda kamati ya uchunguzi kuhusu utendaji kazi wa Meneja"



from MPEKUZI

Comments