RC Makonda ataka shule zifungwe kwa masaa 72

Mkuu wa Dar es salaam, Paul Makonda ameziomba Mamlaka za Elimu kufunga shule kwa siku mbili kufuatia mvua zinazoendelea katika jiji hilo.

RC Makonda ameyasema hayo leo wakati akikagua maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Dar es salaam.

“Nimeziomba Mamlaka za elimu kufunga shule kwa siku mbili, hadi tutakapowaambia siku ya Jumatano kulingana na hali itakavyokuwa kwasababu mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mengi yamejaa mengi kwa hali hii sio salama,” amesema RC Makonda.

Hata hivyo Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,  TMA, imesema mvua kubwa zitaendelea kunyesha mpaka mwezi Mei, mwaka huu, hivyo imewataka watu kuchukua tahadhari mapema.

Pia TMA imeeleza kuwepo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Morogoro, Dar es salaam, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara, Pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Kigoma, Tabora, Katavi, Kilimanjaro, Arusha, na Manyara.

”Kwa Tarehe 16/04/2018 Kuna muendelezo wa tahadhari na Agalizo la Matarajio ya kuwepo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa”.


from MPEKUZI

Comments