Prof. Jay awachana Viongozi wanaopiga picha na wasanii

Mbunge wa Mikumi kupitia CHADEMA ambaye pia ni msanii mkongwe wa hip hop Bongo, Joseph Haule maarufu kwa jina la Profesa Jay, amesema kwamba kitendo cha baadhi ya viongozi kuita wasanii na kupiga nao picha bada ya kuwasaidia matatizo yao si sahihi, kwani wasanii hao wana matatizo makubwa

Akizungumza Bungeni Prof Jay amesema serikali haiwezi kuwa inachukua kodi kwa wasanii bila kuwatengenezea mazingira mazuri ya kazi zao na kutatua changamoto zao, na kuitaka kuweka bajeti maalum kwa ajili yao ili kutatua matatizo yao na sio kuishia kupiga nao picha.

“Huwezi ukamkamua ng'ombe kabla hujamlisha majani, niwaambie serikali wekeni bajeti kwa wasanii, wana matatizo makubwa kuliko hayo mnayodhani, maana mnadhani kuwasaidia wasanii wa Tanzania ni kuwaalika sehemu za maofisini kwenu na kupiga nao picha, kupiga selfie na vitu vingine.

"Wasanii wa Tanzania wana matatizo makubwa, hawahitaji kula ubwabwa na nyinyi, wanahitaji muwasaidie masuala ya kazi zao zinazoibiwa, wanahitaji wasaidiwe wasuala ya masoko, wanahitaji wasadiwe mitaji”, mesema Prof. Jay

Sambamba na hilo Prof. Jay ameitaka BASATA kuwajibika kwenye kuwaelimisha wasanii kama ilivyopewa mamlaka yake, na sio kuwa sehemu ya kutoa hukumu tu pale wanapokosea.


from MPEKUZI

Comments