Watoto wawili wamefariki kwa kugongwa na basi lenye namba za usajili T720 EEV ambalo linafanya safari zake Bukoba kwenda Mwanza na kisha basi hilo kupinduka na kusababisha majeruhi ya watu 20 waliokuwa kwenye basi hilo.
Ajali hiyo imetoka katika Kitongoji cha Katongo kjiji cha Rulanda kata ya Rulanda Wilayani Muleba Mkoani Kagera na gali hilo likapinduka na kusababisha majeruhi ya watu watatu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Rulanda, Evart Erenest amesema kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya asubuhi ambapo watoto hao walikuwa wanavuka barabara wakielekea msikitini.
Amewataja watoto waliofariki ni Muhajiri Abdumajidi mwenye umri wa miaka 6 ambaye ni mkazi wa kata ya Gwanseli pamoja na Abdallah Alidi mwenye umri wa miaka 7 ambaye naye ni mkazi wa kata ya Rulanda.
Aidha abiria waliojeruhiwa wameokolewa na wenzao na wamepelekwa katika hospitali ya Rubya wilayani Muleba mkoani humo.
Hata hivyo, mashuhuda wamesema kuwa sababu kubwa ya ajali hiyo ni hali mbaya ya hewa katika eneo hilo iliyosababishwa mvua zinazoendelea kunyesha.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment