Makonda agharamia mazishi ya Agness Masogange

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amegharamia gharama mbalimbali katika msiba wa Agnes Gerald alimaarufu kama Masogange ambaye amefariki April 20, 2018 na kuzikwa leo April 23, 2018 jijini Mbeya.

Akiongea mbele ya waombolezaji na Mkuu wa mkoa wa Mbeya mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Matebe Mathias 'MC Pilipili' ambaye ndiye 'MC' wa shughuli za mazishi ya Agnes Masogange amesema kuwa wameona mkono wa serikali katika hilo na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ndiye aliyefanikisha na kulipia magari ambayo yamewapeleka wasanii mbalimbali Mbeya.

"Mkuu wa mkoa wa Mbeya kuna upendo mkubwa ambao tumeuona kutoka kwenu kwani ulikuwa karibu na sisi muda mwingi, ulikuwa ukitupigia simu kujua tupo wapi hivyo naamini usiku wa leo hujalala kabisaa. 

"Pia tunamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwani yeye ndiye aliyelipia magari mawili, matatu ambayo yametuleta hapa Mbeya leo kutokea Dar es Salaam, hata kamati ambayo ilikuwa imeandaa kuanzia kutoa heshima ya mwisho pale Leaders Club ambayo ilikuwa chini ya Steve Nyerere ilipewa nguvu na watu wa serikali tumeona serikali mmetupa support vizuri" alisema MC Pilipili

Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla aliweza kuwapokea na kutoa neno la shukrani kwa wasanii na watu mbalimbali ambao wameweka tofauti zao pembeni na kuungana kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha wanampumzisha salama mwenzao katika nyumba ya milele.

"Mueendelee kuwa pamoja hivi hivi bila kujali tofauti zenu, mabifu yenu mzidi kuwa wamoja kwani hili jambo mmejenga heshima kubwa sana, naomba nitoe pole sana kwa familia kwa msiba huu" alisema Makalla


from MPEKUZI

Comments