Kilimo cha Bangi Charuhusiwa Rasmi Zimbabwe

Nchi ya Zimbabwe imehalalisha uzalishaji wa bagi kwa matumizi ya kiafya na kisayansi.

Zimbabwe itakuwa nchi  pili kufanya hivyo barani Afrika baada ya Lesotho, ambayo ilitoa leseni yake ya kwanza kwa kilimo cha mmea huo mwaka uliopita.

Waziri wa afya David Parirenyatwa amechapisha sheria zinazowaruhusu watu na kampuni kupewa leseni ya kufanya kilimo cha bangi ambayo hufahamika nchini humo kama mbanje, na kwamba watu wa nchi hiyo sasa wanaweza kutuma maombi ya kulima bangi, na leseni yake itakuwa inaombwa upya kila baada ya miaka mitano, na itawaruhusu wakulima kumiliki, kusafirisha na kuuza bangi.

Watuma maombi watatakiwa kueleza ni wapi watafanyia kilimo chao, kiwango ambacho wataweza kuzalisha na kuuza na wakati wa kuzalisha bangi hiyo.

Nchini Zimbabwe ilikuwa ni haramu kupanda, kumiliki au kutumia mmea huo nchini Humo, na iwapo mtu atapatikana na makosa hayo anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 12 jela.


from MPEKUZI

Comments