Waziri Mwijage Aweka Jiwe La Msingi La Ujenzi Wa Majengo Ya Viwanda....Mavunde Awataka Wajasiriamali Dodoma Kuchangamkia Mikopo Kutoka Sido

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh Charles Mwijage(MB) ameweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Majengo kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo katika eneo la Kizota-Manispaa ya Dodoma ambapo jumla ya viwanda vidogo 45 vinatazamiwa kuanzishwa kupitia utaratibu wa Clusters “Kongani” na pia kutoa mafunzo kwa Wajasiriamali mbalimbali.

Waziri Mwijage amewataka wanaDodoma kujifunza masuala ya Ujasiriamali kupitia SIDO na kuanzisha Viwanda vidogo kwa sababu Wizara yake imedhamiria kuwainua Wajasiriamali wadogo kuanzisha viwanda vingi vidogo katika kuchochea uchumi wa Viwanda.

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amemshukuru Waziri Mwijage kwa kusimamia upatikanaji wa eneo hilo la ekari 11 ambalo SUMA JKT watajenga **Industrial sheds **za kuweka Viwanda vidogo 45 na hivyo kuinua uchumi wa wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Viwanda.

Mavunde pia amewataka Wajasiriamali wa Jimbo la Dodoma Mjini kuchangamkia fursa za mikopo kupitia mfuko wa uwezeshwaji wajasiriamali(NEDF) uliopo chini ya *SIDO* ili wapate mitaji ya kuanzisha na kuendeleza viwanda.

Naye Lt Col. Mahenge kutoka **SUMA JKT **ameahidi kuifanya kazi hiyo ya ujenzi kwa muda uliokubaliwa na kwa kiwango cha hali ya juu ili majengo hayo yatumike kirahisi kwa kazi iliyokusudiwa.


from MPEKUZI

Comments