Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harisson Mwakyembe leo Machi29, 2018 ametangaza kufuta adhabu ya kufungiwa kwa msanii wa muziki Roma Mkatoliki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam Waziri Mwakyembe amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa Roma Mkatoliki atakuwa huru kufanya shughuli zake za muziki kama ilivyokuwa awali kwa sharti moja la kukamilisha taratibu za kujisajili BASATA.
Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki ambaye naye aliongozana na Waziri Mwakyembe amesema kuwa hata kama ameachiwa huru lakini wimbo wake wa kibamia ataviomba vituo vya redio na runinga kutocheza wimbo huo.
Mwanzoni mwa mwezi Machi serikali kupitia Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia miezi sita msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa kukaidi amri ya kubadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa Kiba100.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment