TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Moja ( 31 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Wakaanza kupigana na ikamlazimu mwenye kipande cha bangi mdomoni kukitema pembeni huku kikiendelea kuwaka na kikaangukia kwenye mafuta ya pretroli yanayotoka kwenye tanki lililo pasuka la gari aina ya Scani ambayo yamesambakaa barabarani na ndani ya dakika mlipuko mkubwa ukatokea na kusababisha idadi kubwa ya watu wanao gombania viroba vya unga na vindoo vya mafuta kurushwa mbali na wengine kupoteza maisha

ENDELEA
Moshi mwangi na harufu kali ya moshi wa mafuta aina ya Petrol ikatawala katika eneo zima la eneo rulilopo huku vilio vikianza kutwala kwa wale walio wapoteza ndugu zao kwenye ajali ya moto.Ikanilazimu kumsogeza madam Zena pembeni zaidi ili kuepuka kuunguo kwa moto unaosambaa kwenye hili eneo kwa kupitia upepo mkali.Gari za Polisi mbili zikafika katika eneo la tukio na sikujua ni nani aliye wataarifu na baada ya muda gari za zima moto na gai ya wagonjwa ikafika katika sehemu ya tukio na kuanza kupakiza baadhi ya wagojwa mahututi ikiwemo madam Zena na wakawahishwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga iitwayo Bombo.

 Msongamano wa magari mengi yaliyo simama kutokana na ajali ikazidi kuongezeka na kusababisha msongamano mkubwa wa magari mengi yanayotoka mkoani na yanayokwenda mkoani.Maiti za wanakijiji walio ungua katika mlipuko zikaanza kukusanywa eneo moja na nikajikuta nikitafuta sehemu nikisimama kutokana na kushindwa kuiangalia miili ya watu wengine kwa maana imeharibika kiasi kwamba inatisha.Hadi inafika saa tatu usiku magari yakaanza kuruhusiwa kuendelea na safari baada ya magari yaliyo pata ajali kusogezwa barabarani.

Nikarudi kijijini na kukuta nyumba nyingi zikiwa zimetawaliwa na vilio kiasi kwamba hata raha ya viroba vya unga na vindoo vya mafuta ya kupikia ikawa imetoweka miongoni mwa wanakijiji wengi,Kutokana sikuwa mwenyeji kwenye kijiji hichi mojo kwa moja nikafikizia kwa bibi aliye nihudumia kipindi nikiwa nimeokotwa porini,akanipatia chakula nikala na kwenda kuoga kasha nikarudi ndani na kumkuta akichanganya changanya dawa zake kama kawaida

“Unajisikiaje sasa mjukuu wangu?”
“Kdogo afadhali bibi yangu”
“Mshukuru Mungu kwa yale yote yaliyo tokea na ameweza kukuokoa hadi ukafikia kuwa na hali kama hiyo”
“Ni kweli bibi na vipi mbona hauendi kwenye misiba?”
“Mbona hiyo sio misiba mjukuu wangu”
“Sio misiba kivipi bibi?”
“Mjukuu wangu kwenye ulimwengu huu kuna mambo mengi sana ambayo wanadamu huwa tunayapitia na kuyafanya,Yakiwemo mazuri na mabaya”
“Ni kweli bibi ila sijakuelewa ni kwanini umesema kuwa sio misiba?”
“Watu hao hawajafa kilicho tokea kwenye hiyo ajali ni kiini macho tu ila watu wanao sadikika kufa kwenye hiyo ajali wote wapo hai”
Nikajihisi kama mwili ukiwa umesizi kidogo huku nikifikiria cha kumuuliza bibi kwa maana ninacho kisikia hapa ni kama vile nipo ndotoni vile na ikanilazimu kuamini ninacho ambiwa hapa ni kweli na wala sio ndoto

“Kwa nini bibi?”
“Kwa malezo zaidi nitakufwata usiku nikakuonyesha hao watu sehemu walipo”
“Usiku kivipi?”
Bibi akanyanyuka na kuingia ndani kwake na kuniacha na alama ya kuuliza huku mapigo ya moyo yakiaanza kunienda mbio hata hamu ya kulala ikaanza kunitoweka.Nikatoka nje kwa kunyata na nikafanikiwa na kukuta bado wenye misiba wakiendelea kupiga makalee ya kuomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.Nikaanza kutembea kuelekea barabarani na kukuta  na watu wengine wakiendelea kusafisha safisha barabara huku gari aina ya Rosa iliyo pata ajali ilinyanyuliwa na gari maalumu lenye winchi na kuwekwa barabarani
“Kaka hili gai lenu munalipeleka wapi?”
Nilimuuliza mmoja wa wafanyakazi walio kuwa wakijishuhulisha na jinsi ya kuinyanyua gari hii ya abiria
“Tanga mjini”
“Samahani kaka sijui ninaweza kupata japo kanafasi ka kujishikiza na hadi huku munapo elekea?”
“Kwani wewe unakwenda wapi?”
“Mimi ninakwenda Tanga mjini?”
“Sasa huku ilikuwaje ukaja?”



from MPEKUZI

Comments