TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Tatu ( 43 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Nikaanza kushangulia huku nikiruka ruka juu, nikaanza kupiga hatua nikiondoka baharini huku nikiwa nimejawa na furaha sana.Gafla nikasutkisha nikastukia nikirushwa juu na nikiwa angani nikalishuhudia joka likiwa limeufumbua mdomo wake, huku likiningojea niingie ndai ya kinywa chake.Nikaanza kurudi chini kwa kasi kubwa huku nikipiga kelele nyigi na moja kwa moja nikaingia ndani ya mdomo wa joka

ENDELEA
Kwa, haraka nikachomo mshale ulipo kwenye podo langu nililo livaa mgongoni, Nikiwa ninaendela kushuka katika tumbo la mwili wangu, huku nikiwa nimeibana pumzi yangu.Nikaukita mshale wangu kwenye tumbo la joka hili na kuanza kuuchana mwili wake huku nikimshale wangu kwenye tumbo la joka hili na kuanza kuuchana mwili wake huku nikiwa ninaendelea kushuka nao chini hadina kumfanya joka hili kuanza kubingiria bingiria huku maji mengi, ya bahari yakiwa yanakingia mwilini mwake
Wingi wa maji unao ingia mwilini mwa joka, yakanifanya niweza kupata nafasi ya kutoka nje ya joka hili ambalo bado linaendela kutapa tapa kwenye maji huku likitoa ukelele mkali.Jokaa likaanza kufutuka huku likiwa moto mkali, Kwa bahati mbaya likanipiga kikumbo, kwa kutumia mkia wake kilichorusha mbali na eneo alilo kuwepo na kunitoa nje ya bahari na kwabahai mbaya nikangukia kwenye kisiki cha mti wa mkono, na kutulia tuli huku giza zito likitawala macho yangu

  ***
 “Eddy......Eddy”
Kwa mbali niliisikia sauti ya Rahma ikiniita,nikayafumbau macho yangu taratibu na kukutana  na mwanga mkali ulio nipiga kwenye macho yangu, huku nikiwa, nimelala kwenye kitanda nikipelekwa nisipo pajua na pembeni yangu akiwepo Rahma naye akionekana akitembea huku machozi yakimwagika.Kila ninapojaribu kuyafumbua macho yangu, nikajikuta nikiona maruweruwe hata watu wanao kisukuma kitanda nilicho kilalia sikuweza kuwaona vizuri.Nikajikuta nikitawaliwa tena na giza kwenye macho yangu, na sikuelewa kilicho endelea.

Macho yangu yakaanza kupata mwangaza tena wakuona mwanga, nikajaribu kuyapitisha pitiasha kwenye kila kona ya chumba na kufanikiwa kutambua kuwa hapa nilipo ni hospitalini.Pembeni ya kitanda changu, kuna meza ndogo, na juu yake imejaa maua mengi pamoja na kadi nyingi, sikujua ni nani aliye ziweka, kwenye mkono wangu wa kushoto nimechomekwa mrija unaodondosha maji taratibu kwenye mishipa yangu.Tumboni kwangu kumefungwa bandeji lililo kaza, lililo zunguka sehemu nzima ya tumbo hadi mgongoni.Nikaiona kadi moja iliyo andikwa maandishi makubwa kwa kalamu ya wino
(Eddy tunakupenda sana endelea kuugua pole,MUNGU atakuponya)

Nikaunyoosha mkono wangu na kuchukua moja ya kadi na kulifungua ndani na kukuta maandishi yanayo nitakia mimi kuugua pole.Mlango ukafunguliwa na akaingia nesi akiwa amevalia mavazi mazuri.Baada ya kuniona akaachia tabasamu pana
“Habari yako kaka Eddy?”
“Salama mambo?”
“Salama, karibu tena duniani”
“Duniani kivipi?”
“Ni story ndefu, ila kwa muda huu pumzika kwanza”
“Sawa, ila Rahma wangu yupo wapi?”
“Amekwenda kupata chakula cha mchana”
“Kwani nesi, hapa nipo wapi?”
“Upo hospitali ya mkoa, Bombo”
“Sawa, ila ninaomba kama una namba ya Rahma mpigie”
“Usijali kwa hilo, kaka yangu”



from MPEKUZI

Comments