TANESCO Yakanusha......"Hakuna Tatizo Lolote Katika Mfumo wa LUKU"

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)limekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii  inayodai kutakuwa na tatizo katika mfumo wa manunuzi ya LUKU kuanzia Machi 25 hadi Aprili 5 mwaka huu.

Taarifa hiyo ya kutunga inadai kutokana na hali hiyo wateja wanunue umeme wa kutosha katika kipindi hicho.

Tanesco kupitia Ofisi ya Uhusiano imesema taarifa hizo si za kweli na uzushi wenye nia ya kupotosha umma kwani haijatokea taarifa yoyote kuhusu hitilafu katika mifumo ya manunuzi ya LUKU.

"Ikumbukwe kwamba taarifa kutoka Tanesco hazitolewi na mtu binafsi bali ofisi ya uhusiano iliyo chini idara ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo ni msimamizi wa utoaji taarifa za shirika hili,"imesema taarifa ya Tanesco.

Imewaomba wateja wote wa Tanesco waipuuze taarifa hiyo kwani haina ukweli wowote ."Wateja wote mnaombwa kuendelea kutumia huduma za umeme kama kawaida."


from MPEKUZI

Comments