Peter Lujuakali, Susan Kiwanga na Wafuasi 55 CHADEMA Mahakamani Tena Leo

Wabunge wa Chadema, Susan Kiwanga (Mlimba) na Peter Lijualikali wa Kilombero na wafuasi wengine 55 wa chama hicho wamefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro kusikiliza kesi inayowakabili.

Huku wakiwa na wakili wao, Fred Kalonga wabunge hao wamefika mahakamani hapo leo asubuhi Machi 28, 2018.

Kwa pamoja wanakabiliwa na na mashtaka manane  ikiwemo kuharibu mali katika uchaguzi mdogo wa marudio wa udiwani kata ya Sofi, Novemba 26, 2017 katika Wilaya ya Malinyi mkoani humo


from MPEKUZI

Comments