Mchungaji Msigwa aunganishwa katika Kesi ya Akina Mbowe na Viongozi Wengine

Wakili wa viongozi wa Chadema, Frederick Kihwelo amesema mbunge wa chama hicho Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa naye ameungwanishwa na viongozi waliowekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.

Kihwelo amesema Mchungaji Msigwa aliitwa na alipofika polisi naye aliunganishwa na wenzake.

Viongozi hao wamefutiwa dhamana kwa kuwa wanapotakiwa kuripoti polisi, baadhi yao hushindwa kutokea.

Viongozi waliowekwa mahabusu ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.


from MPEKUZI

Comments