Takribani wiki mbili zilizopita Dogo Janja aliingia katika headlines hasa katika stori za kidaku mara baada ya kutokea katika video ya ngoma yake ‘Wayu Wayu’ akiwa na muonekana wa kike.
Kitendo hicho kilizua mjadala mpana kiasi katika music industry kwa hapa Bongo. Sasa Rapper Nikki Mbishi hajawa nyuma katika hilo, kupitia ukurasa wa twitter Nikki ameandika; Dogo Janja ni “VIDEO QUEEN” .
Baada ya tweet hiyo Dogo Janja amejibu; Chupa Lako Ukinihitaji Onana Na Management bei yangu SIO GHALI SANA.
Jibu hilo linaweza kutafsiriwa kuwa Dogo Janja yupo tayari kufanya hivyo katika video ya Nikki au msanii yeyote ila kinachotakiwa ni kuonana na menejimenti yake kwa ajili ya malipo kitu ambacho mwishoni amesisitiza sio ghali.
Madee ambaye anafanya kazi na Dogo Janja kupitia Tip Top Connection anatajwa kuwa ndiye alimpatia Janjaro idea ya video hiyo. Madee alikaririwa akisema idea hiyo alitaka kuitumia katika video yake ila hakuwa na wimbo wa kutoa hivi karibuni ndipo akaitoa kwa dogo Janja.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment