China yasema Korea Kaskazini Imekubali kuondoa silaha za nyuklia

China imesema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amethibitisha katika ziara yake ya siri huko Beijing kuwa yuko tayari kuondosha silaha za nyuklia katika rasi ya Korea na kushiriki katika mazungumzo yatakayo zishirikisha Korea Kusini na Marekani.

Shirika la habari la China Xinhua, lililoweka picha za kiongozi wa Korea Kaskazini akiwa na Rais wa China Xi Jinping, limeripoti kuwa Kim na mkewe Ri Sol Ju walifanya ziara ya kiserikali Beijing kuanzia Jumapili hadi Jumatano, na alihudhuria karamu maalum katika ukumbi wa Great Hall of the People akiwa na Xi na mkewe Peng Liyuan.

Wakati wa mkutano wao viongozi hao wawili walisisitiza umuhimu wa kuendeleza umoja wa karibu kati ya China-Korea Kaskazini ambao ulikuwa umeingiliwa na mvutano juu ya Pyongyang kukaidi na kuendeleza jaribio la silaha za nyuklia na makombora ya balistika.

Xi alikuwa amewafiki vikwazo vizito vilivyokuwa vimewekwa chini ya usimamizi wa Marekani ili kumshinikiza Kim kurejea tena katika mazungumzo na kuacha kutumia vitisho vya programu yake ya nyuklia ikiwa ni suluhisho la kumaliza vikwazo vya kiuchumi, kuongeza misaada na kuwahakikishia usalama wao.

Katika miezi michache iliyopita, Kim alibadilisha msimamo wake wa kukataa mazungumzo alipotangaza Korea Kaskazini ni taifa lenye silaha za nyuklia.

Baadae alibadilisha msimamo huo na kupunguza mvutano kwa kusimamisha majaribio ya nyuklia na makombora, kuiacha nchi yake kushiriki katika michezo ya Olympic huko Korea Kusini na kuwa tayari kufanya mazungumzo ya suala la nyuklia pamoja na Rais wa Korea Kusini Moon-Jae-in ambao umepangwa kufanyika April, na mkutano mwengine na Rais wa Marekani Donald Trump unaotarajiwa kufanyika May 2018.

Kim amemwambia Xi kuwa yuko tayari kutafuta ufumbuzi wa “suala al kuondoa nyuklia” muda wa kuwa Korea Kusini na Marekani “watakuwa tayari kushiriki katika juhudi hizi kwa nia njema, kuweka mazingira ya amani na utulivu, wakati akichukua hatua za kusukuma mbele mazungumzo hayo na kufikia muwafaka ili kufikia amani,” kwa mujibu wa Xinhua.


from MPEKUZI

Comments