CAG Aomba Radhi Kuhusu Taarifa ya Ukaguzi Aliyoiwasilisha kwa Rais Magufuli

Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Profesa. Mussa Assad ameomba radhi wananchi na serikali juu ya taarifa ya deni la taifa na kusema kuwa yalifanyika makosa ya kimatamshi, deni hilo ni himilivu.

Profesa Assad ametoa taarifa hiyo mjini Dodoma ambapo amesema deni halisi ni shilingi trillion 46.08 na ni himilivu hivyo anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wananchi na taasisi za serikali.

CAG wakati akitoa ripoti hiyo kwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu suala la muenendo wa deni la taifa alidai kuwa deni la taifa si himilivu lakini kwa mujibu wa utafiti ambao wamefanya wao CAG ameibuka na kuomba radhi na kusisitiza kuwa ripoti ya CAG ni siri hadi itakapowasilishwa bungeni. 


from MPEKUZI

Comments