Breaking News: Mahakama Yawaachia Kwa Dhamana ya Milioni 20 Kila Mmoja Viuongozi 6 wa CHADEMA Wakiongozwa na Mbowe

Leo March 29, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa masharti ya dhamana kwa viongozi 6 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe kwa kuwa na wadhamini 2 kila mshtakiwa atakayesaini Bondi ya Shilingi Milioni 20.

Pia wadhamini hao wawe na barua za utambulisho, ambapo baada ya kutimizwa masharti hayo Mbowe na wenzake wawe wanaripoti Central Police mara moja kwa wiki.

Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi ameieleza Mahakama ya Kisutu kuwa watakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo kutoa masharti ya dhamana kwa Mbowe na wenzake


from MPEKUZI

Comments