Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, (Bavicha) Patric Ole Sosopi, amesema Serikali ya awamu ya tano ina lengo la kuifuta Chadema.
Akizungumza leo, Machi 31, katika mkutano na wanahabari uliofanyika katika ofisi za chama hicho, Sosopi amesema, wapo watu wanaotumwa na Serikali kuichafua Chadema na kupata sababu ya kukifuta chama hicho.
“Tumewapuuza kwa muda mrefu, tukiamini vyombo vitachukua hatua dhidi yake lakini kwa kuwa wanamtuma anaendelea kuwa salama,” amesema.
Amesema Chadema inawahakikishia Watanzania kuwa jitihada za kuifuta Chadema hazitafanikiwa na hakuna yeyote atakayeifuta Chadema.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment