Baada ya kumsifia Irene Uwoya, Msami adai hamjui Dogo Janja

Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja inazidi kugonga vichwa vya habari, safari hii msanii Msamii aliyekuwa mpenzi wa Irene hapo awali anatajwa sana katika ndoa hiyo.

Msanii na Irene wameacha maswali mengi baada ya hivi karibuni kuanza kusifiana katika mitandao kitu ambacho baadhi ya watu wanadai hakileti picha nzuri katika ndoa ya Irene na Dogo Janja.

Sasa muimbaji huyo akizungumza na E-Newz, EATV amesema yeye amejua na Irene kwa kipindi kirefu hivyo hata kama mrembo huyo amejuana na mtu mwingine si sababu ya wao kushindwa kuendelea kuwa marafiki.

“Naichukulia kawaida sana, nikikujua leo baada ya miaka mitano mbele ukajuana na mtu mwingine, mkawa na maisha mengine mimi nakujua wewe huyo mtu mwingine simjui,” amesema.

“Kwa hiyo ni vitu ambavyo haviwezi kupotea tu, kwanini nianze kupotezea kwamba yule sasa hivi yupo na fulani sitakiwi kuongea naye, maisha hayako hivyo” ameongeza.

Hata hivyo ameonya kuwa Irene siyo mke wake na anatambua kuwa ni mke wa mtu.


from MPEKUZI

Comments