MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-
0657072588
ILIPOISHIA
Kabla Marima hajamalizia sentensi yake tukasikia kontena kiligongwa gongwa, kwa haraka Marima akajichomoa kwenye jogoo wangu, akatafuta rimoti ya Tv liyopo humu ndani, akawasha Tv ambayo inaonyesha mandhari ya nje. Tukawaona askari usalama barabarani wanne, wawili wakiwa pembeni ya kontena. Mmoja akizungumza na dereva akimuamrisha afungue kontena watazame ni mzigo gani walio upakiza, huku askari mmoja mmoja akiwa amesimama kwenye mlango wa kontena akitazama tazama tazama mlango, jambo lililo mfanya Marim kuchukua bastola yake na kuinyooshea kwenye mlango wa kontena tayari kwa shambulizi litakalo tokea mbele yake.
ENDELEA
Nikamuona dereva akishuka kwenye gari huku akizungumza na askari aliye muamrisha kushuka. Uzuri wa gari hili limetegwa kamera nje ambazo s rahisi kwa mtu kuweza kuziona na ndizo zinazo tusaidia kuona kila knacho endelea nje.
Dereva akarudi nyuma ya gari na kumkuta askari mwengine aliye kuwa anatazama tazama nyuma ya hili gari. Taratibu dereva akaanza kufungua kufuli la kwanza, jambo lililo nifanya niichukue bastola yangu, huku nikiwa makini san.
“Ngoja kwanza tuzungumze”
Askari mmoja alizungumza huku akimzuia dereva kufungua nyuma ya gari, ikambidi dereva kumuangalia askari huyo, wakanong’onezana kwa muda kisha dereva akatoa waleti yake mfukoni na kuto noti tano za shilingi elfu kumi kisha akamkabidhi askari mmoja aliye tazama kila sehemu kisha pesa hiyo akaiweka mfukoni mwake. Akamruhusu dereva kufunga kufuli la gari kisha, akamruhusu dereva kuendelea na safari yake. Sote tukarudi kukaa kwenye sofa huku tukitabasamu kwa maana mchezo wetu ulikatishwa katikati.
“Hii nchi bwana”
Marim alizungumza huku akiniwekea mguu wangu mmoja kwenye paja langu.
“Ina nini?”
“Rushwa inanuka bado, japo raisi anajitahidi kupambana nayo”
“Yaa ndio hivyo, ila Mungu akibariki itakuja kuisha”
“Sio kwa nchi hii”
“Ok. Tuendelee”
“Ahaa stimu wala sina kabisa, wamenichefua hawa askari”
“Poa, ehee hembu niambie ilikuwaje kuwaje hadi ukawa kama ulivyo kuwa?”
“Ahaa ni stori ndefu sana, yaani ile simu uliyo niachia ilbadilisha maisha yangu yote”
“Kivipi?”
“lle simu nyuma si kulikuwa na kijidue kimebandikwa”
“Ndio”
“Basi mim nilikitoa kwa sasababu nikaona kama kinanichafulia pozi. Nakumbuka siku ile niliyo tekwa nilikuwa nimekwenda chuo kuna maswala nilikuwa ninayafwatilia. Sasa nilipo kuwa ninatoka, ikaja gari moja kali. BMW X6, akashuka dada mmoja mrembo akaniita, akiomba aniulize kitu”
“Ehee”
“Najuta hata kwa nini nilimfwata, nilistukia kitu chenye ncha kali akinigusa nacho, nakumbuka kalikuwa ni kajisindano. Kalinipa usingi nikajikuta nikiingia ndani ya gari hilo mimi mwenyewe, kuanzia hapo sikujua hata ni wapi ninapo elekea”
“Huyo dada ulendelea kumuona?”
“Huyo aliye nichoma kisindano?”
“Ndio”
“Si Yudia, mamaee zake yule dada, alinivurugia ndoto zangu zote”
“Ehehee ikawaje?”
Marima akamaa vizuri huku kwenye sofa, huku akinitazama usoni mwangu.
“Mimi kuja kuzinduka nilijikuta nipo kwenye moja ya bonge la meli. Humu ndani kuna viwanja vya kufanyia mazoezi yaani kusema kweli hakuna kutoroka, na hiyo sehemu hilo limeli lilipo kumezungukwa na papa wakali, yaani wale wanao kufa mazoezini, wala hakuna haja ya kuzika, wanatupwa tu baharini, ndani ya sekunde tu unaona jinsi anavyo gawanyishwa gawanyishwa vipande vipande”
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment