AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 51 na 52 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA                      
ILIPOISHIA 

Nikasikia Monica akimuambia mzee huyo anahitaji hati, mzee huyo akampatia bahasha, Monica huku simu akiwa ameibana sikioni mwake, akatoa hati ya nyumba.
“Ni hati yenyewe?”
“Ndio ni hati nyenyewe?”
“Ina jina gani?”
“Raja Bahamuz”
“Ok mpatie mtoto wake”
Nilipo hakikisha Monica amekabidhiwa kila kitu nikasimama sehemu niliyo kuwa nimelala nikilifwatilia tukio hilo.
“Nyoosha mikono yako juu na bastola yako itupe pembeni”
Niliisikia sauti ya K2 nyuma yangu, jambo lililo nifanya mwili mzima kunisisimka kwa hasira kali
  
ENDELEA
Taratibu nikanyoosha mikono yangu juu, huku bastola yangu nikiitupia pembeni.
“Geuka nyuma”
Alizungumza kwa ukali, nikafanya kama alivyo hitaji niweze kufanya. Taratibu nikageuka huku nikimtazama usoni. Alipo niona ni mimi akabaki akiwa ameduwaa, macho yamemtoka, nikahisi hata nguvu za mwili zimemuishia.

“Halloo K2”  
Nilizungumza huku nikimtazama kwa macho ya dharau. Nikaitazama mikono yake nikaiona jinsi inavyo tetemeka kwa woga, nikatambua kwamba hii ndio nafasi yangu ya kuweza kumshambulia. Pasipo kufikiria kwa maya ya pili nikajituma hewani huku nikirusha teke lililo elekea maeneoa ya mikono ya K2 na bastola yake ikaangukia pembeni. Hapo ndipo K2 alipo jipanga kwa kukabiliana na mimi woga na wasiwasi ukamtoka. Akaanza kurusha ngumi za huhakikia ambazo nyingi katika hizo niliweza kuzikwepa japo kuna baadhi ya ngumi hizo zilinipiga kwenye baadhi ya mwili wangu.
‘Hakikisha unarudi na kichwa cha K2 hapa’
Kauli ya mama ikanirudia kichwani mwangu, roho ya kinyama ikaniingia moyoni mwangu. Nikaanza kujibu mashambulizi ya K2 kwa kasi kubwa na nguvu. Ngumi zangu kwa wakati huu ninaimani zimeongezeka uzito, kila ngumi niliyo mpiga iliweza kumyumbisha.

    Gafla nikaanza kusikia milio ya risasi ikitokea uwanjani, nikageuza macho yangu na kuona kundi la wana kikosi cha NSS, walio valia suti nyeusi wakija kwa kasi. Nikampiga mtama mmoja K2 na kuanguka chini, na kuanza kubingiria kwenye ngazi za uwanja huu. Kwa haraka nikaifwata bastola yangu ilipo huku nikiwa ninaruka sarakasi zilizo nisaidia sana kuweza kukwepa risasi za wezangu hawa ambao kwa sasa tumekua kama maadui.
Nilipo hakikisha bastola yangu nimeishika vizuri mkononi, sikuwa na haja ya kuanedelea kukaa katika eneo hili, kwa kupitia sehemu niliyo ingilia katika uwanja huu, ndio njia ninayo tumia kutoka. Nikashuka kwenye ukuta huo kwa haraka na kusimama nje. Nikatazama gari langu sehemu lilipo sikuliona hapo wasiwasi ndipo ulipo anza kunikabili.

“Ingia kwenye gari”
Niliisikia sauti ya Monica akizungumza pembeni yangu huku akiwa amesimamisha gari langu pembeni yangu,    nikamtazama kwa sekunde kadhaa kisha nikaingia kwenye gari, na akaliondoa kwa kasi katika eneo hili.
“Ulikuwa umekwenda wapi?”
Nilizungumza huku nikiwa ninatazama nyuma kuangalia kama kuna gari ambazi zinatufwata.
“Nilichukua gari kuliweka sawa kwa maana nilisha kuona umewekwa kwenye ulinzi”
“Ulijuaje kama ningeweza kutoroka eneo lile?”
“Unaonekena ni kijana shupavu, sio mtu wa kukamatwa kiurahisi rahisi kiasi kile, tena na mwanamke”
Manano ya Monica kidogo yakanitatanisha akilini mwangu, nikawaza labda alihitaji kuondoka na gari langu na kubadilisha mawazo yake, ubaya niliufunga mlango na kuondoka na funguo zangu.

“Funguo za gari ulizipatia wapi?”
“Nilizikuta nje ya gari zimeanguka”
Nikajipapasa sehemu nilipo kuwa nimeziweka na ni kweli sikuzioona.
“Sasa tunaelekea wapi?”
Nilimuuliza Monica ambaye yupo makini barabarani akizidi kuongeza mwendo kasi wa gari.
“Tunaelekea nyumbani kwangu”
“Ni wapi?”
“Wewe twende utapaona”
Monica hakusimamisha gari, tukafika maeneo ya Jaje, akazidi kusonga mbele kueleka maeneo ya Pangani. Katikati ya msitu akakunja kushoto mwa barabara ambapo kuna barabara ndogo inayo ruhusu gari kuweza kupita. Tukazidi kusonga mbele, kidogo wasiwasi ukaanza kunipata, bastola yangu nikaishika vizuri endapo kutatokea jambo lolote la hatari basi ninaweza kujitetea.



from MPEKUZI

Comments