Updates: Zitto Kabwe Kaachiwa kwa Dhamana

Mbunge Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana leo asubuhi  baada ya kushikiliwa katika kituo kikuu cha Polisi mkoani humo tangu jana usiku. 

Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo alikuwa kwenye ziara ya chama chake mkoani humo.

Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya milioni 50 na amedhaminiwa na Wakili wake, ndugu Emmanuel Lazarus Mvula. Ametakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi 12, 2018.


from MPEKUZI

Comments