Treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania iliyokuwa ikitokea mkoani Dodoma kwenda Kigoma imepata ajali katika eneo la Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza.
Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na kusababisha mabehewa mawili kuanguka katika dimbwi dogo la maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Othieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Mpaka sasa hakuna taarifa ya vifo wala idadi ya majeruhi.
Behewa kadhaa bado zimesalia kwenye njia yake baada ya ajali.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment