AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“NAHITAJI SIRI HII UITUNZE NA USIMWAMBIE BINADAMU WA AINA YOYOTE NA LAITI UKIDHUBUTU KUMWAMBIA MWANADAMU KUWA UMEKUTANA NA MIMI NITAITOA ROHO YAKO UMENIELEWA……?”
“Ndi….ooo”
“Na kingine nitahitaji uwe rafiki yangu”
“Siwez….”
Kabla hata sijaimaliza sentensi yangu nikajikuta akinisukuma na kunikandamiza ukutani huku mkono wake akiwa umenikaba kwenye koo lango na nikaanza kuhisi roho yangu ikitaka kunitoka kwani ananguvu nyingi na kingine kinachozidi kuniogopesha ni macho yake kaunza kuwaka moto huku akitokwa na machozi ya damu
ENDELEA
“Katika maisha yangu haijawahi binadamu wa aina yoyote kunikataa”
Olvia Hitler alizungumza na sauti nzinto iliyo nifanya nizidi kuogopa,kisha akaniachia na nibaki nikiwa nina elea elea angani.Sura yake ikarudi katika hali yake ya kawaida huku akiwa ananitazama kwa tabasamu zuri
“Eddy narudia tena kuzungumza mimi sio kiumbe mbaya wa kuwadhuru wanadamu ila ninauwezo wa kumdhuru yule tu anaye hitaji mimi nimfanyie hivyo……Nahitaji kukufanya kuwa mtu maarufu na anaye fahamika sana Tanzania na Duniani kwa ujumla”
“Ki…v…ipi?”
“Sawali zuri,kwanza unatakiwa usiniogope.Pili unatakiwa kufwata zile amri zangu nitakazo kupa na nilizo kupa……Natambua sana moyo wako unampenda Rahma japo huyo mwnamke mchafu anakufanya ummsaliti…..Kutokana hukuwa unajua ni kitu gani kinachoendelea kwa leo nitakusamehe ila kwa sharti moja tu nahitaji ummuamshe huyo mwanamke na aende zake kwake wakati huu kisha ndio nitaendelea na mazungumzo na wewe”
“Sa..sawaa”
Nilizungumza kwa kigugumizi kisha taratibu akanirudisha kitandani na gafla akapotea na hali ya chumba ikarudi kama kawaida na nikajikuta nimekaa kitandani huku shuka likiwa limenifunika kuanzia miguuni hadi kwenye kiunoni,Nikamtazama Halda mwenzangu hana hata analo lijua ndio kwanza ananazidi kukoroma kiasi kwamba nikaanza kujipa moyo labda inaweza ikawa ndoto.Nikaanza kumtingisha Halda huku nikiliita jina lake hadi akaamka na kukaa kama nilivyo kaa mimi huku akipiga miyayo ya usingizi
“Nakuomba uvae uende kwako”
“Eddy”
“Wewe ninakuomba uvae uende kwako sasa hivi”
“Eddy umechanganyikiwa?”
“Sijachanganyikiwa nina akili zangu ni nzima kama unavyo niona ila nakuomba tuu uvae na uenda kwako kama kulala tutalala siku nyingine”
“Eddy kama unaota nakuomba uniache mimi nilale shughuli uliyo nipa ni kubwa sawa mpenzi wangu”
Halda alizungumza huku ikijilaza tena kitandani na kunifanya nimuamshe kwa nguvu hadi akaanza kukasirika
“Eddy saa tisa yote hii unataka mimi niende wapi mwanaume gai huna huruma au unataka usiku huu nikabakwe huko barabarani?”
“Kama utabakwa ukiwa ndani ya gari basi ila ninacho taka mimi vaa nguo zako uende zako kwako sitaki matatizo na mpenzi wangu”
“Eddy siondoki”
“Kumbuka upo kwangu?”
“Hata kama ila siondoki lije WINCHI,TREKTA au KATAPILA haliwezi kuning’oa hapa kitandani na wala siondoki”
“Hilda unanijua tena vizuri? Sihitaji nikubamize ndio uondoke”
“Eddy nipige,nikate kate,nivunje vunje,nisage sage ila mimi siondoki NG’OO”
Nikazidi kuchanganyikiwa kwani Halda hakutaka kabisa kusikia kitu kinacho itwa kuondoka ikanilazimu kushuka kitandani na kujifaunga taulo langu na kumbukumbu ya maji aliypo nipa bibi ikanijia kichwani nikakaumbuka nimeyaweka jikoni
“Unakwenda wapi sasa?”
“Wewe lala kama hutaki kuondoka niache”
“Sasa Eddy huko nje usiku huu unapo kwenda untaka kwenda kufanyaje?”
“Kwani nimekuambia ninakwenda nje hembu lala huko”
“Nakufwata”
Halda akanyanyuka kitandani huku akiwa ameijifunga shuka na kuanza kunifwata jikoni ninapo elekea,Nikaikuta chupa ya maji katika sehemu niliyo iweka kaisha taratibu nikayatoa kwenye kifuko cheusi nilipo kuwa nimeyaweka
“Sasa hayo maji ni ya kazi gani?’
“Hilda hembu niache wewe rudi chumbani kalale”
“Mmmm haya mwaya kama ndio uchawi wa kwenu kunywa maji ya Dasani usiku wa manae”
Halda alizungumza huku akirudi zake chumbani kwangu,nikamchungulia na kuona tayari ameingia ndani kwangu na kuufunga mlango.Nikapiga hatua za kwenda nje nikashika kitasa cha mlango na kufungua.Moyo ukanipasuka kiasi kwamba nikajikuta natamani kuzirai kwanik eneo zima la nje ya nyumba yangu nikakuta ni bahari tena yenye maji mengi huku Olvian Hitler akiwa amekaa kwenye kiti cha dhahabu huku pembeni yake kukiwa na wasichana wawili wanao mpepea kwa mikia ya Simba iliyo tengenezwa vizuri huku wakiwa juu ya maji
“Eddy nashindwa kuamini kama mwanamke huyo umeshindwa kumtoa ndani kwako”
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment