Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 03 na 04

Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
***ilipoishia***

wachawi wachawi wenzake walimpokea kwa furaha...bi'chenda alizipiga hatu mpaka kwa mkuu wa wachawi na kumkabidhi mtoto huyo mchanga sherehe kubwa ikafanyika usiku huohuo....walicheza ngoma za kichawi huku wakila nyama za binadamu....ghafla mkuu wa wachawi akapaza sauti na kusema,,"Tusikilizane......kijiji kizima kikawa kimya kisha akazipiga hatua huku kambeba doto...akapanda na kusimama juu kwenye mgongo wa binadamu waliyemchukuwa kichawi usiku huo kwaajili ya kumfanya jukwaa la kumkuu wa wachawi..kisha akasema...........

***Endelea***
Siku ya leo,,,ni siku ambayo itakuwa ni yenye baraka kubwa katika kijiji chetu....mtoto huyu mchanga....ameteuliwa na miungu ya kuzimu....wachawi wengine wakaanza kupiga makofi huku wakiongea Lugha ambayo haina maneno ya kibantu..
(lugha isiyokuwa rasmi.haieleweki)..kisha mkuu wa wachawi akachukua kisu pamoja na sumu ya nyoka iliyochanganywa na dawa ya kichawi..akamchana doto kiunoni kwa kutumia kisu hicho kisha..akachukua ile sumu ya nyoka iliyochanganywa na dawa ya kichawi akampaka kwenye jeraha hilo kililokuwa likitoa Damu....

kutokana na maumivu makali Doto alilia kwa mfululizo bila kunyamaza....kisha mkuu wa wachawi akamteuwa mwanamke mmoja aliyekuwa anamtoto anayemnyonyesha miongoni mwa wachawi wa kijiji hicho..(GAMBOSHI) akamkabidhi Ili awe anamnyonyesha Doto pamoja na kumlea... mlaka atakapofikisha umri wa kuitumikia kazi ya miungu wa kuzimu rasmi..baada ya kumaliza sherehe hiyo..wachawi walitawanyika,,,kila mmoja alipanda kwenye ungo wake na kutoweka kimiujiza...
Bi'chenda ajajitokeza chumbani mwake...akavua ile kaniki nyeusi..pamoja na irizi zake mbili akaziweka kwenye kimkoba chake,,kisha akaweka ndani ya begi na kufunga zipu ya begi..akapanda kitandani akaanza kuutafuta usingizi..

******************
asubuhi palipokucha alionekana Rose akiwa ameketi kitandani huku macho uamevimba kutokana na kulia usiku kucha....Rose hakuweza kabisa kuoata usingizi usiku wa jana...Seba alikuwa na kazi kubwa ya kumbembeleza mkewe usiku kucha...wlikesha bila kutarajia.....
ghafla mlango wa chumbani ukagongwa......seba akanyanyuka,,akazipiga harua kwenda kufungua mlango...... alipofungua alimuona mama yake Bi'chenda akiwa amebeba beseni lililokuwa na maji ya moto ndani yake kwa ajili ya kumkanda Rose sehemu zake za siri.... seba aliamua kutoka nje ya chumba ili kumpisha mama yake akamkande mkwe wake..

Bi'chenda alijifanya kumbembeleza rose akimsihi anyamaze huku akisema,,"nyamaza mwanangu ni mipango ya Mungu...atakujalia utapata watoto tena usilie.... Rose alimtazama mama mkwe wake kwa huzuni huku akionekana kufarijika na maneno hayo akasema"asante mama yangu...kisha akavua nguo na kulala chali kitandani....bi'chenda akaanza kumkanda..



from MPEKUZI

Comments