Polisi wamtia mbaroni Mama anayetuhumiwa kumuua Mwanae na kumzika

Msichana mwenye umri wa miaka 25, Anastazia Elias, mkazi wa Kata ya Kipindu wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amenusurika kifo baada ya kuokolewa na polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.
 
Wananchi wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua mwanawe wa kiume baada ya kujifungua ambapo alimviringisha na vipande vya khanga na kumuweka kwenye kikapu alichokificha chini ya uvungu wa kitanda chake.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Kipundu kilichopo mjini Namanyere.
 
Kamanda Kyando amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi wilaya Nkasi na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio kukamilika. Wakizungumza baadhi ya wanawake  wamedai mtoto huyo alizikwa juzi usiku katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba ambayo mama yake mzazi anaishi na bibi yake.
 


from MPEKUZI

Comments