Mwili wa Akwilina ulivyochukuliwa Muhimbili kupelekwa NIT kuagwa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa aliongoza msafara wa magari, likiwemo lililobeba mwili wa  mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuelekea katika viwanja vya chuo hicho kwa ajili ya kuagwa.

Jeneza lenye mwili wa mwanafunzi lilikuwa  katika gari maalumu la kubebea maiti.

Baada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo, saa 10 jioni safari kuelekea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwa mazishi itaanza. Akwilina atazikwa kesho


from MPEKUZI

Comments