Msajili wa Vyama vya Siasa Aiweka Kitanzini CHADEMA.....Awaandikia Barua Kuwata Wajieleze Kwa Kufanya Vurugu na Maandamano

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema barua hiyo ya msajili waliipokea jana na wanapaswa kuijibu kabla ya Februari 25, 2018.

Chadema waliandamana Februari 16 mwaka huu wakishinikiza kupewa viapo vya mawakala wao kabla ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni.


from MPEKUZI

Comments