MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Tukatoka na kuanza kutembea kwenye kordo huku K2 akiwa amenishika kiuno, kabla hata hatujafika mlango wa kutokea mama Mariam akatoka chumbani kwake, alipo nitazama akakunja sura yake akionekana kuchukizwa na tukio hilo la K2 kunishika kiuno, hata kabla hatujasonga mbele, mlango wa mbele ukafunguliwa na akaingia Mariam akiwa ameshika kifuko cheusi, aliopo muona K2 akajikuta akiangusha kifuko chake na kumfanya K2 kunitazama na macho ya kuniuliza swali juu ya tukio analo liona kwa wanawake hawa wawili.
ENDELEA
Nikamshika K2 na kutoka naye nje, nikamsindikiza hadi kwenye gari. Nikasalimiana na Hassani aliye anza kunipa pole, juu ya tukio lililo toke.
“Sasa Dany hakikisha kwamba mukianza safari unaipigia simu”
“Sawa bosi”
Nilimuita bosi kutokana na uwepo wa Hassani. K2 akanikonyeza pasipo Hassani kuona kisha akaingia kwenye gari. Wakaondoka eneo la mtaani kwetu, na kuniacha nikilisindikiza gari hilo kwa macho tu, nikageuka nyuma yangu na kufungua geti na kuingia ndani, ila ninakutana na Mama Mariam akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia ndani. Nikapandisha vingazi na kuufwata mlango.
“Naomba kupita”
“Ninamazungumzo na wewe fanya tuzungumze”
“Tuzungumze sasa hivi kwa maana hapa ninajisikia vibaya”
Nilizungumza huku nikimuonyesha mama Mariam majeraha ya kwenye viganja vyangu, akavitazana na nikaiona sura yake ikijikunja kidogo akionekana kuguswa na maumivu hayo.
“Umefanyaje?”
“Nimeungua jana kwenye nyumba ya mzee Jongo”
“Mungu wangu, ilikuwaje sasa?”
Mama Mariam alizungumza huku akisogea pembeni ya mlango, tukasogea mlangoni hapo. Kutokana nyumba yetu imezungushiwa geti sikuona aibu ya kufungua vifungo vya shati langu na kulivua. Nikamuonyesha kidonda nilicho ungua mgongoni.
“Yesu wangu. Dany ni wewe?”
“Ndio”
“Jamani sasa mbona hukuniambia, wakati namba yangu unayo?”
“Nilikuwa hospitali usiku wa kuamkia leo”
“Masikini wee, pole jamani.”
Mama Mariam alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa simanzi ndani yake. Nikalivaa shati langu naamini hata lengo la mama Mariam kuweza kuniuliza juu ya K2 kwa hali ya ukali imemuisha.
“Sasa Dany umekula?”
“Hapana”
“Ngoja nimuambie Mariam akuhesabu chakula, kwa maana anapika wali maharage”
“Ahh sawa”
“Alafu Dany yule uliye toka naye ni nani kwako?”
“Yule ni bosi wangu, amekuja kunitembelea na kuniletea barua ya mapumziko”
“Ahaaa kwa maana nilihisi ni mwanamke wako alivyo kuwa amekushika kiuno”
“Hapana sio mwanamke wangu”
“Basi nenda kapumzike, badae nitakuja ndani kwako”
“Sawa”
Nikatangulia kuingia ndani na kumuacha mama Mariam akiwa amesimama hapo kibarazani. Nikaingia ndani kwangu, cha kwanza kukifanya ni kuanza kuzihesabu pesa hizo alizo nipa K2. Nikajikuta furaha ikunitawala, taratibu nikaanza kupanga nguo chache ambazo ninaweza kwenda kuzitumia nyumbani Tanga nitakapo kwenda. Nilipo maliza kuziweka kwenye kibegi kidogo, nikatoa pesa kadhaa na kuziweka kwenye begi hilo kisha nyingine ninaziweka kwenye suruali ambayo nitasafiria kesho.
Muda ukazidi kwenda, huku nikiwa ninatazama miziki kwenye luninga. Majira ya saa mbili mlango ukagongwa na ninaisikia sauti ya Mariam, nikamruhusu aweze kuingia ndani. Akaingia akiwa amebeba sahani iliyo jaa ubwabwa na maharage, huku pembeni akiwa ameweka samaki mkubwa aliye kaangwa na kachumbari.
“Karibu chakula Dany”
“Asante, mbona umenijazia chakula”
“Nataka ule ushibe, usiku nitakuja”
Mariam alizungumza huku akitabasamu. Akachota maji kwenye ndoo iliyopo humu ndani kwangu kisha akachukua beseni na kutaka kuninawisha.
“Nipatie kijiko tu si unaoviganja vyangu jinsi vilivyo”
“Nimeviona ila nawa kidogo, utamlaje huyo samaki”
“Haya mwaya”
Akaninawisha mkono wa kulia, kisha akanipatia kijiko. Nikiwa ninachota wali huo, akanipokonye kijiko akakishika na kunilisha, kisha akakata kipande cha samaki akakiweka mdomoni mwake na kunisogezea mdomoni mwangu, sikuwa na jinsi zaidi ya kukipokea. Kwa mara ya kwanza Mariam akaninyonya mate kwa ridhaa yake.
“Ngoja nitoke mama asije akanifikiria vibaya bure”
“Poa ila leo usiku usije, si unajua tena sipo vizuri”
“Mmmm jamani Dany?”
“Yaa usije naomba nipumzike, kesho nina safari ya kwenda Tanga kusalimia”
“Kwa hiyo hadi urudi ndio tutafanya jamani?”
“Usijali sikai sana”
“Haya mwaya
Marim akanibusu tena mdomoni na kutoka chumbani kwangu, nikashusha pumzi kidogo kwa maana mchezo ambao Mariam anataka kuufanya ninahisi ipo siku mambo yanaweza kuwa mabaya, pale mama yake akifahamu na anaonekana ni mama mwneye wivu sana na mpenzi wake japo hatujayaanza kwa makubaliano.
Nikaendelea kula chakula taratibu hadi nikakimaliza, nikabeba sahani hiyo na kutoka nayo nje, nikamkuta Mariam anaosha vyombo.
“Asante chakula chako kitamu sana”
“Asante”
Mariam alizungumza huku akinipokea sahani hiyo. Akanikonyeza na mimi nikaondoka na kumuacha aendelee na kazi yake. Nikaingia ndani kwangu na kukuta mwanga wa simu yangu iliyopo mezani ukizima ikiashia kwamba kuna mtu amepiga au kutuma meseji, nikiwa nje. Nikaichukua na kuminya pembeni na kuifanya simu kuwaka mwanga wake, nikaingiza namba za siri ninazo ziweka kwenye simu yangu, ilipo waka nikafungua ujumbe wa meseji ambao unatoka kwa mama Mariam.
(DANY NITAKUJA SAA SITA USIKU USIFUNGE MLANGO EHEE)
(Sawa)
Nikamjibu na simu yangu kuirudisha mezani, nikavua nguo zangu na kujifunga taulo. Nikachukua sabuni yangu na kutoka ndani kwangu. Niakakutana na Mariam mlangoni akiwa amebeba dishi la vyombo.
“Unakwenda kuoga?”
Aliniuliza kwa sauti ya chini huku akitazama nyuma kama kuna mtu
“Ndio”
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment