AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 09 na 10)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA      

Lucy alizungumza mara baada ya kuniona nikiwa ninashangaa shangaa. Tukaingia kwenye lifti japo ni nyumba ya gorofa moja ila ina lifti yake. Tukafika juu, nikakuta seble nyingine hii ikiwa imeizidi seble ya chini mara dufu.
“Hichi ndio chumba utakacho kuwa unakitumia kwa maagizo ya baba kama jinsi alivyo sema”
Nikaingia kwenye chumba hicho, kwa jinsi kilivyo kikubwa kikanifanya nibaki nimeduwaa.
“Njoo nikuonyeshe kitu”
Lucy alizungumza huku akielekea kwenye mlango mmoja ulipo ndani ya chumba hicho, akaufugua na kuingia ndani na mimi name nikaingia ndani.
“Hili ni bafu, sinki hilo la kuogea lote limetengenezwa na dhahabu hata hayo mabomba unayo yaona hapo pembeni yametengenezwa na dhahabu”
Lucy alizungumza, kitendo cha yeye kugeuka na kunitazama, usoni tukagonda vifua na kujikuta chocho zake zilizo simama vizuri zikigusana na kifua change kilicho jengeka vizuri kwa mazoezi.

ENDELEA
“Ahaa am sorry”
Lucy alizungumza huku akitazama chini kwa aibu, akataka kusogea pembeni ila nikamuwahi kumshika kiuno. Tukatazama usoni kwa dakika kadhaa, nikamuona jinsi Lucy anavyo tetemeka kwa woga kwenye midomo yake inayo chezacheza.
“Dany”
“Mmmm”
Lucy akaka kimya baada ya mimi kuitikia hakujibu kitu chochote, nikamsogeza karibu kabisa na mwili wangu, miili yetu ikagusana kabisa. Lucy akazidi kutetemeka na kujikuta akifumba macho na kushindwa kunitazama kabisa usoni mwangu.

Nikasogeza lipsi zangu taratibu hadi zikagusana na lipsi zake. Lucy akakunja kabisa sura yake na kuyapandisha mabega yake juu kidogo akionekana kuogopa sana kwa kitu ambacho ninataka kukifanya. Nikameza mate kidogo  kisha nikarudisha kichwa changu nyuma na kumuachia mkono.
Nikaendelea kutazama bafu hilo lililo tengenezwa vizuri sana, akilini mwangu ninakwaza juu ya utajiri wa mzee Jongo, akiwa kama mtumishi wa serikali japo yupo ngazi ya juu, ila pesa zote hizi amezitolea wapi. Lucy akatoka bafunu humo pasipo kunisemesha kitu cha aina yoyote. Ikanibidi na mimi kutoka, sikumkuta pia katika chumba hichi.

“Amekwenda wapi huyu?”
Nilizungumza huku nikielekea mlangoni, nikafungua na kumuona akiingia kwenye moja ya chumba kilichomo huku juu gorofani.
“Anatatizo gani huyu?”
Nilijiuliza huku nikielekea kwenye chumba hicho, nikakuta mlango ameurudishia tu na kuna kijiupenyo kidogo ambacho unaweza kuona ndani. Nikausukuma taratibu na kuchungulia ndani. Nikamuona Lucy akiwa amekaa kitandani huku akimwagikwa na machozi usoni mwake.
‘Ina maana amechukizwa na kumkiss?’
 Ikanibidi kuingia chumbani humo, Lucy akanyanyua kichwa chake. Kwa ishara ya mkono akanionyesha ishara ya kutoka chumbani humo.

“Lucy kuna tatizo lolote jamani?”
“Nimesema ondoka chumbani kwangu”
Hapo Lucy alizungumza kwa hasira hadi nikabaki nikiwa nimemkodolea macho kwa maana sikutarajia msicha mzuri kama huyu anaweza kukasirika kwa namna hii.
“Lakini Lucy si…..”
“Koma kuniita jina langu, sitaki mazoea na wewe, hata kama umeniokoa na moto ila masikini kama wewe huwezi kuwa na mimi”
Maneno ya Lucy yakapenya moja kwa moja kwenye moyo wangu. Nikamtazama Lucy kwa macho yaliyo jaa uchungu, nikajikuta nikianza kujutia moyoni mwangu ni kwa nini nimejitia kwenye majaribu ya kumsaidia hadi leo sehemu ya mgongo wangu imepatwa na majeraha.

“Look at yourself. Do you think unaweza kuwa na msichana kama mimi ehee”
Lucy alizidi kuzungumza kwa dharau huku akinitazama usoni mwangu. Akanipandisha kwa macho na kunishusha kisha akaachia msunyo mkali ulio anza kunipandisha hasira.
“Let me tell you this. Wewe sio level yangu, na siwezi kuwa na wanaume wa Sinza kama wewe. Toka chumbani kwangu kabla sijakufanya kitu mbaya”
“Asante”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga. Nikatoka chumbani kwake, sikuona hata haja ya kurudi katika chumba nilicho ambiwa nitakaa humo. Sikutumia lifti iliyopo ndani humo, nikaanza kushuka kwenye ngazi za chumba hicho kwa haraka, nikatoka nje ya nyumba hicho. Nikafika getini mlinzi akanifungulia huku akinitazama usoni kwa kunishangaa kwa maana machozi yalisha anza kunilenge lenga. Ubaya wa huku Masaki, pikipiki wala bajaji hazipiti piti mitaani, ikanibidi kuanza kutembea hadi kwenye kituo cha dalala, nikakodi pikipiki, dereva akanipeleka hadi Sinza ninapo ishi.

“Nisubiri nikuletee pesa yako”
“Sawa bosi”
Nikaingia ndani, moja kwa moja nikaelekea chumbani kwangu, kitu kilicho nistua kidogo ni kuukuta mlango wangu upo wazi kidogo. Nikakumbuka kwamba jana sikuweza kuufunga na funguo ila niliuurudishia tu.
Nikaingia kwa kuusukuma taratibu. Macho yakanitoka baada ya kumkuta K2 akiwa amelala kitandani huku amejifunga taulo kiunoni mwake na amelala kifudi fudi.
Sikumstua chochote zaidi ya kuchukua pesa kwenye waleti yangu iliyokuwa kwenye sofa, nikatoka nje na kumlipa dereva bodaboda na kurudi chumbani kwangu.
   Nikamtazama jinsi K2 alivyo lala kitandani na makalio yake yalivyo ju. Nikatamani hata kuchukua mkanda na kuyacharaza pasipo uruma ila heshima ya kazi nikajikuta ikinivaa taratibu nikajikuta nikimgusa mgongoni na kumtingisha.
“Bosi, Bosi”
“Mmmmm”
K2 alizungumza huku akijigeuza taratibu. Akanitazama usoni mwangu, akaachia tabasamu pana kidogo.
“Umerudi?”
“Ndio, umekuja kufanyaje chumbani kwangu?”
“Kwani kuna ubaya wa mpenzi kuja nyumbani kwa mpenzi wake”
K2 alizungumza huku akikaa kitako kitandani, kwa jinsi ninavyo mtazama usoni mwake nikatamani kumtandika kofi kama alili nipiga jana asubihi, ila nikajikuta nikibaki nimemkazia macho. K2 akanitazama mikononi na kuishika kwa haraka na kuitazama.



from MPEKUZI

Comments