MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Afande ninaomba nimpigie mwanasheria wangu aje kituoni?”
Nilizungumza tukiwa njiani. Askari huyo hakuweza kunijibu chochote zaidi ya kunikata jicho baya. Tukafika kituo cha polisi. Wakanifungua pingu, wakaniamuru kuvua mkanda, viatu, kutoa waleti mfukoni. Nikafanya hivyo kitu lilicho mstusha askari aliye kuwa akinipapasa ni bastola yangu niliyo kuwa nimeichomeka kiunoni.
“Jamani huyu ni jambazi”
Askari huyo aliuzungumza kwa sauti ya juu na kuwafanya askari wengine wote kituoni kunitazama mimi huku wengine walio na bunduki kuninyooshea mimi, huku wakiniamuru kunyoosha mikono juu kwa ukali sana.
ENDELEA
Nikafwata kama wanavyo hitaji, nikainyoosha mikono yangu juu huku nikimtazama askari aliye nichomoa bastola yangu.
“Piga magoti wewe mjinga”
Askari mwengine alisisitiza kwa sauti ya ukali, taratibu nikapiga magoti. Askari huyo akachuka waleti yangu na kuifungua, akaanza kuikagua vitambulisho vyangu. Nikamuona akistuka baada ya kutoa kitambulisho changu cha kazi. Akanitazama mara mbili mbili huku macho yakimtoka na jasho likimwagika.
“Kuna nini kinacho endelea hapa”
Nilisikia sauti ya kike, nyuma yangu. Ikanibidi kugeuka na kumkuta mkuu wa polisi ambaye ninamtambua ni rafiki wakaribu sana na K2 na mara nyingi niliweza kumuona akija ofisini kwetu.
“Mkuu kuna huyu kijana alifanya fujo, ndio tumemleta hapa kituoni”
Mwanamama huyo mrefu kwenda juu, aliye valia suruali ya kaki pamoja na shati la kaki, lenye nyota kadhaa kwenye bega lake, akazunguka na kuja kusimama mbele yangu.
“Mumegundua nini?”
Alimuuliza askari aliye shika kitambulisho changu. Askari huyo akaonekana kupata kigugumizi na kujikuta mkuu wake akikichukua kitambulisho hicho na kukikoma. Akanitazama kwa haraka kisha akayarudisha macho yake kwenye kitambulisho hicho.
“Nani aliwapa oda ya kwenda kumkamata?”
Askari wote wakaka kimya. Kila mmoja alimtazama mwenzake, mwanamama huyo kwa ishara akaniomba ninyanyuke juu. Nikannyanyuka na kuwafanya askari wote kuduwaa.
“Mrudishieni kila kitu chake, unatoa toa macho ya nini?”
Askari aliye chukua waleti na bastola yangu, akanirudishia huku mwili mzima ukimtemeka. Sikulijali juu ya woga nikachukua kila kitu changu, nikavaa mkanda pamoja na viatu vyangu.
“Samahani kijana, naomba tukayazungumze ofisini kwangu”
Mwana mama huyo alizungumza huku akinitazama. Nilipo maliza kufunga kamba za viatu vyangu, nikaongozana naye hadi kwenye ofisi yake iliyopo gorofani. Akanikaribisha kwenye kiti kilichopo mbele ya meza yake kisha yeye akaka kwenye kiti kilichopo nyuma ya meza yake hiyo yenye mafaili mengi pamoja na meza ya mezani na simu ya upepo.
“Samahani kwa usumbufu wa vijana wangu, naona walikuchukua pasipo kujua kwamba wewe ni nani”
“Kwa hilo halina tabu, ni vyema nikaondoka na kwenda kuripoti kazini kwangu kwamba kazi yangu iliziwa na vijana wako”
“Hapana hapana, wachukulie ni vijana wezako wale. Endapo wataingia kwenye tabu wengine ndio kwanza hata pesa ya serikali hawajaitafuna”
“Kwa hiyo na mimi nikafukuzwe kazi kwa ajili ya vijana wako, unatambua kabisa kazi yangu ilivyo na uhatari wa hali ya juu, ila bado vijana wako wakaamu kuniharibia ndio nini sasa”
Nilizungumza kwa kumkoromea mama huyo baada ya kugundua amingiwa na hofu kidogo.
“Basi ngoja niweza kuzungumza na bosi wako, ili kukukingia kifua, si unajua tena sote sisi ni watumishi wa uma na kazi yetu ni moja”
Mama huyo alizungumza huku akichomoa simu yake aina ya Samsung Galaxy note 3. Akaminya minya baadhi ya namba ambazo sikuziona na kuiweka simu yake sikioni huku akinitazama usoni.
“Shosti vipi?”
“Safi vipi”
Kutokana na simu hiyo kuwa na sauti kubwa kidogo niliweza kuisikia sauti ya K2, nikatamani kumpokonya simu mama huyo ila nikajikuta nikishindwa na kubaki nikiwa nimemkazia macho.
“Safi tu, bwana nina ombi moja”
‘Ombi gani?’
“Kuna kijana wako hapa alikamatwa na vijana wangu akiwa kwenye kazi yake wakidai alifanya vurugu kwenye moja ya ofisi sasa nikaona nikujulishe mapema isije akaja huko ukawajibisha”
‘Anaitwa nani?’
“Anaitwa Daniel Thamson Kajenge”
‘Mmmmm’
“Mbona unaguna sasa?”
‘Hapana, upo naye hapo au amesha ondoka?’
“Nipo naye hapa ofisini kwangu”
‘Hembu mpatie simu’
Mama huyo akanipatia simu yake, taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Hallo”
“Hivi Dany unachanganyikiwa siku hizi?”
K2 alizungumza kwa ukali na kunifanya nimtazama mama huyo kwa jicho la kuiba nikagundua anayafwatila mazungumzo yangu kwa umakini.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment