Ni rahisi sana kwa shabiki kindakindaki wa mpira wa miguu kuwa mchawi katika maisha halisi kuliko shabiki kindaki ndaki wa muziki.
Hii ni kwa sababu shabiki wa timu moja ya mpira wa miguu hawezi kuwa shabiki wa timu nyingine ya mpira wa miguu ambayo inashiriki katika ligi moja na timu yake .
Kwa mfano Shabiki wa Yanga hawezi kuwa shabiki wa Simba wala kufurahishwa na mafanikio ya Simba kama ambavyo Shabiki wa Simba hawezi kuwa shabiki wa Yanga wala kufurahishwa na mafanikio ya Yanga.
Shabiki wa Real Madrid hawezi kuwa shabiki wa Barcelona wala kufurahishwa na mafanikio ya Barcelona na kinyume chake.
Ili hali katika upenzi wa muziki hali ni tofauti sana. Shabiki wa Msondo Ngoma ana weza kupendezwa na nyimbo za wana Sikinde Ngoma ya Ukae kama ambavyo shabiki kindakindaki wa wana Sikinginde Ngoma ya Ukae anavyo weza kufurahishwa na nyimbo za Msondo Ngoma.
Shabiki kindaki ndaki wa Diamond Platnumz anaweza kuwa mpenzi mkubwa sana wa nyimbo za Ali Kiba kama ambavyo Shabiki wa damu wa Ali Kiba anavyo weza kuwa mpenzi mkubwa wa nyimbo za Diamond Platnumz.
Shabiki kindakindaki wa Davido anaweza kuwa mpenzi wa kutupwa wa nyimbo za Wizkid kama ambavyo shabiki wa kutupwa wa Wizkid anavyo weza kuwa mpenzi mkubwa wa nyimbo za Davido.
Shabiki kindaki ndaki w a AKA anaweza kuwa mpenzi wa kutupa wa nyimbo za Casper Nyovest kama ambavyo shabiki wa damu wa Casper Nyovest anavyoweza kuwa mpenzi mkubwa wa nyimbo za AKA.
Shabiki kindakindaki wa Tupac Shakur anaweza kuwa mpenzi wa damu wa nyimbo za Notorious BIG kama ambavyo shabiki kindakindaki wa Notorious BIG anavyo weza kuwa mpenzi wa damu w a nyimbo za Tupac Shakur.
Lakini hali ni tofauti sana kwa mashabiki wa mpira wa miguu. Ushabiki wa mpira wa miguu unapo tamalaki unaweza kunmfanya shabiki husika akawa na tabia ama hulka ambazo hazina tofauti na hulka za wachawi.
Kitendo cha shabiki wa timu moja kutofurahishwa na mafanikio ya timu nyingine ambayo haya iathiri timu yake hakina tofauti yoyote na mchawi ama mshirikina ambae anaumizwa kwa sababu mtoto wa jirani yake amefaulu na kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu.
Mfano mzuri ninao kwa shabiki mmoja wa mpira wa miguu ambae jina na mahali anapotoka nina muhifadhi.
Shabiki huyu alinipigia simu yangu juzi na kunieleza kwa uchungu mkubwa sana kuwa yeye ni shabiki wa kufa wa klabu ya Arsenal na kwamba ameumizwa sana na kitendo cha mchezaji Sanchez kuuzwa kwenda Manchester United.
Shabiki huyo akaendelea kunieleza kama ifuatavyo :
"NATAKA UMFUNGE SANCHEZ. FUNGA MIGUU YAKE, AKIENDA MAN U ASIFUNGE HATA GOLI MOJA. FUNGA AKILI YAKE AKIWA UWANJANI ASAHAU KAMA YUPO UWANJANI . FUNGA KUMBUKUMBU ZAKE AKIFIKA GOLINI ASAHAU GOLI LILIPO. MTIE MALIENGE KWENYE MACHO YAKE AKIWA NA MPIRA AWE ANAONA GOLI LIKO PEMBENI APIGE PEMBENI NA KUKOSA GOLI. GOLI PEKEE AMBALO ATATAKIWA KUFUNGA LIWE GOLI LA KUJIFUNGA MWENYEWE NA SI VINGINEVYO.
MFARAKANISHE NA WACHEZAJI WENZAKE, KOCHA WAKE NA MASHABIKI WAKE. NA MWISHO WA SIKU ATUPIWE VIRAGO NA KUONDOKA KWA AIBU.. MFICHE UWANJANI ASIONEKANE UWANJANI. AU MTIE MAJERUHI , AUMIE KWENYE MAZOEZI KABLA YA KUANZA KUITUMIKIA KLABU YAKE AKAE AKIWA MAJERUHI KWA MSIMU MZIMA NA TIMU YAKE IMCHOKE NA KUMTUPIA VIRAGO ..ASIONEKANE UWANJANI NA KAMA IKITOKEA BAHATI MBAYA AMEONEKANA UWANJANI BASI AONEKANE AKIWA AMEKAA KWENYE BENCHI NA IKITOKEA AKICHEZA MECHI BASI TIMU YAKE IFUNGWE MAGOLI MENGI NA AWE NI MTU WA KUKOSA MAGOLI MARA ZOTE… NIPO TAYARI KWA LOLOTE DOKTA . NINAKUOMBA SANA DOKTA UNISAIDIE KWA HILO”
Shabiki huyu aliongea mambo mengi sana kwa uchungu mkubwa sana.
Maneno ya shabiki huyu wa mpira wa miguu yalinirudisha miaka sita nyuma. Nikakumbuka mwaka 2012 Robin Van Persie alivyo hamia Man U kutoka Arsenal, mashabiki wengi sana wa Arsenal hawakufurahishwa na mmoja kati ya mashabiki hao alinitafuta na kuniambia :
“ DOKTA. , MIMI NI SHABIKI MKUBWA SANA WA ARSENAL. MIMI NI MFANYAKAZI,. OFISINI KWETU KUNA WAFANYAKAZI WENZETU WAWILI MASHABIKI WA MAN U AMBAO WANA DHARAU SANA NA MANENO YA KEJELI SANA HASA TIMU YANGU YA ARSENAL INAPOKUWA IMEFUNGWA. MIMI NINAOMBA UFANYE DAWA ZAKO HAWA JAMAA WAFUKUZWE KAZI AU WAHAMISHIWE KWENYE MIKOA YA MBALI KABISA. ILI NISIWAONE WAKIWA WANAFURAHIA MAGOLI YANAYO FUNGWA NA VAN PERSIE AKIWA AMEVAA JEZI YA MAN U.
NINAJUA VAN PERSIE NI MCHEZAJI HATARI SANA NA SITAKUWA TAYARI HATA KIDOGO KUWAONA FULANI NA FULANI ( ANATAJA MAJINA YAO ) WAKIWA WANAFURAHIA USHINDI W A TIMU YAO KWA MAGOLI YALIYO FUNGWA NA VAN PERSIE. NITAUMIA SANA “
Kwa Mifano hiyo miwili unaweza kuona mahali ambapo ushabiki wa mpira wa miguu una weza kukufikisha.
Katika ulimwengu wa michezo ni jambo la kawaida sana kwa shabiki wa timu Fulani kutofurahi pindi timu yake inapo fungwa au kupata matokeo mabaya . SIna tatizo katika hili.
Ninacho kisema hapa ni pale wewe shabiki wa mpira wa miguu unapofikia hatua ya kuichukia timu pinzani kiasi cha kutofurahishwa na mafanikio ya timu hiyo pinzani hata kama haya kuathiri au kuiathiri timu yako kwa chochote.
Hiyo ndio tunayo ita roho ya kichawi na uchawi.
Mfano mzuri ni huu hapa. Wewe ni shabiki wa Arsenal, timu yako imefuzu kuingia NNe bora na umesha maliza mechi zako zote. Wapinzani wako Man U wamebakiza mechi moja tu na wanatakiwa wapate pointi tatu ili nao waweze kufuzu kuingia nne bora. Bahati nzuri Man U wanashinda na kuingia nne bora. Wewe shabiki wa Arsenal unachukia na kukasirika kabisa kwa sababu Man U na wao wamefuzu kuingia nne bora. Unapofikia katika hatua hii ndipo unapokuwa katika levo moja na wachawi kwa sababu wachawi pia hawapendi kuuona mafanikio ya watu wengine hata kama hayawa athiri kwa chochote..
Ukitafakari suala hili kwa jicho la tatu utagundua kuwa chuki uliyo nayo dhidi ya mafanikio ya timu pinzani mara nyingi huwa ni chuki dhidi ndugu, jamaa, na marafiki zako. Hii ni kwasababu ifuatayo :
“ MARA ZOTE SHABIKI WA TIMU FULANI ANAPO CHUKIZWA NA MAFANIKIO YA TIMU PINZANI HUWA ANAKUWA HACHUKIZWI NA MAFANIKIO YA WACHEZAJI AU TIMU HIYO PINZANI BALI HUWA ANACHUKIA KUONA JIRANI, JAMAA, AU NDUGU NA MARAFIKI ZAKE AMBAO NI MASHABIKI WA TIMU HIYO PINZANI WAKIWA WANAFURAHIA MAFANIKIO YA TIMU HIYO PINZANI NA SI VINGINEVYO “
Kwa hiyo chuki yako wewe sio chuki dhidi ya timu pinzani, ila ni chuki dhidi ya jirani yako unaeonana nae kila siku ambae ni shabiki wa timu pinzani. Hutaki kumuona akiwa anafurahia na unafurahia kumuona akiwa anahuzunika pindi timu yake pinzani inapo pata matokeo mabaya.
Roho au hulka hiyo haina tofauti na roho ya kichawi. Mfano, mwanzoni mwa miaka ya tisini kuna kijana mmoja kutoka mkoa mmoja wa hapa hapa Tanzania, baada ya kuhitimu masomo yake, alipangiwa kufanya kazi kwenye tarafa moja iliyopo katika mkoa mwingine hapahapa nchini.
Tarafa hiyo inasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya magwiji wa uchawi na ushirikina na ipo tofauti kabisa na kata nyingine zote zilizopo katika mji huo ambao ni miongoni mwa miji yenye maendeleo makubwa hapa nchini.
Wazazi wa kijana huyo walimuhasa atakapo fika katika tarafa hiyo, awe na nidhamu na heshima ya hali ya juu sana. Awaheshimu watu wote bila kujali hali zao kimaisha au umri
wao na kikubwa zaidi, awaheshimu sana wazee.
Huyo kijana baada ya kupangiwa kazi kwenye tarafa hiyo, wazazi wake walimuhasa akifika katika tarafa hiyo awaheshimu watu wote, wakubwa kwa wadogo, asiwe na dharau na kikubwa zaidi awe na ukaribu sana na wazee.
Hao wazee ndio watakuwa baba zake ambao watamlinda na kumuongoza na kumfanya aishi salama katika tarafa hiyo. ( KATIKA TARAFA HIYO WAZEE WANAHESHIMIKA SANA NA HUWA HAWAITWI “BABU” BALI BABA )
Kijana alipofika katika tarafa hiyo akaanza kufuata maelekezo aliyo elekezwa na wazazi. Alikuwa na heshima ya hali ya juu sana. Ndani ya muda mfupi tu akawa ameshajulikana kwa magwiji wa tarafa hiyo. Kijana alikuwa akipata mshahara wake, atanunua sukari, chumvi, mchele , sabuni na vitu vingine na kuwagawia magwiji wa tarafa hiyo. Nadhani alikuwa muumini wa methali isemayo “ Mchawi mpe mwana akulelee “, isipokuwa tu yeye aliamua kujikabidhi yeye mwenyewe wamlee. “
Kila siku jioni ilikuwa lazima aende kuripoti kwa wazee hao kama ishara ya kuonyesha heshima, adabu na utiifu kwao. Siku ambayo hakuripoti basi kulikuwa na sababu isiyo weza kuzuiliwa na binadamu na akionana nao kesho yake lazima awaombe radhi.
Kijana huyu alikuwa mjasiriamali pia. Akiwa katika tarafa hiyo akagundua fursa kubwa ya biashara ya mbao na vifaa vya ujenzi pamoja na udalali wa viwanja na mashamba kwa sababu mji ulikuwa unapanuka na watu wengi walikuwa wana jenga kwa kasi.
Jamaa akaenda kuchukua mkopo benki na kuingia kwenye biashara ya mbao ambayo haikuchelewa kuanza kumlipa.
Kijana akawa anatengeneza pesa za kutosha na hata matunzo kwa wale ‘magwiji’ yakaongezeka.
Baada ya kipindi kichache Yule kijana akaanza kuwaambia magwiji hao sentensi ambazo hawakuzipenda.
Hawakupendezwa na sentesi hizo kwa sababu zilikuwa na maana mbaya sana katika tafsiri ya kamusi ya kichawi.
Labda tu kwa wasio fahamu, wachawi wana kamusi yao. Moja kati ya kazi za kamusi ya kichawi ni pamoja na kutafsiri maneno, ishara na vitendo mbalimbali vinavyo fanywa na watu mbalimbali.
Nyuma ya kila sentensi unayo izungumza, huwa kuna sentesi nyingine ya kichawi. Nyuma ya kila kitendo unacho weza kukifanya huwa sentensi ya kichawi.
Kwa mfano : “ A “ ni Kijana mwenye umri wa miaka 25. Kijana huyu amezaliwa na kukulia kwenye kijiji “ X “. Kijiji hiki ni kijiji ambacho wakazi wake wengi ni wachawi na washirikina.
Ndani ya kijiji hiki hakuna maendeleo. Watoto wa kike na kiume kutoka katika kijiji hiki wote wameharibikiwa na hakuna alietoka katika maisha hata mmoja.
Kwa bahati nzuri au mbaya huyu kijana “ A “ baba ake alikuwa na mwamko w a elimu, akampeleka “ A “ kwenye shule za bweni ambako ameweza kusoma kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu. Alikuwa anarudi kijijini kimya kimya kusalimia kisha anarudi mjini kuendelea na masomo yake.
Baada ya kuhitimu Chuo Kikuu, siku moja “ A “ anaenda kutembelea kijijini kwao. Na kwa bahati mbaya au nzuri “ A “ anakutana na mzee “ Y “. Huyu ni mzee ambae anaheshimika na kuogopeka sana hapo kijijini kwa sababu "ugwiji " na “ A “ anamfahamu fika mzee huyu tangu akingali mdogo.
Kwa sababu kijana “ A “ amelelewa katika mazingira ya heshima, anapokutana na mzee “ Y “ kijana huyu anamsalimia kwa heshima na adabu zote na kama hiyo haitoshi, A anamsaidia mzee “ Y “ kubeba mzigo wake , hadi nyumbani kwa mzee “ Y “
Hapo Kijana “ A “ atafarijika moyoni kwamba nimetengeneza sifa ya kuwa kijana mzuri kwa adabu na heshima niliyo muonyesha mzee huyu.
" A " anajiona yupo salama na kwamba ametengeneza urafiki na mzee " Y " .
Lakini kwa mzee “ Y “ ambae ni mchawi na mshirikina yeye atakitafisiri kitendo cha kijana “A “ kwa namna tofauti sana. Akitafsiri kwa kutumia kamusi ya wachawi.
Atakitafsiri kitendo cha kijana “ A “ kama ifuatavyo :
“ DUH! YANI HUYU KIJANA WA MZEE “ X “ PAMOJA NA KUWA NA UMRI WA MIAKA 25 LAKINI AMENIONYESHA HESHIMA NA ADABU YA HALI YA JUU KIASI HIKI?
HAIWEZEKANI HATA KIDOGO. KIJANA WA MIAKA 25 ANANIONYESHA HESHIMA NA ADABU KUBWA KIASI HIKI. INA MAANA BADO TU HAJAHARIBIKIWA?!!! INA MAANA HAVUTI BANG1!!! SIO MLEVI WALA HANA MAKUNDI!!! HAIWEZEKANI !!! SIWEZI KUKUBALI UPUUZI HUU HATA KIDOGO!!!
MIMI AMBAE SIO BABA AKE WALA SINA UNDUGU NAE AMENIONYESHA ADABU NA HESHIMA KUBWA KIASI HICHO, WAKATI WATOTO WANGU WA KUZAA MWENYEWE WENYE UMRI SAWA NA WAKE, WAKIKUTANA NA MIMI WANANIPIGA VIKUMBO, KAMA HIYO HAITOSHI HUWA WANANITUKANA HADI TUSI LA MAMA NA KIPIGO JUU!!!.INA MAANA HUYU KIJANA” A” BADO HAJA HARIBIKIWA ? KAMA MIMI TU AMBAE SIO BABA AKE AMENIONYESHA HESHIMA KUBWA NAMNA HII, VIPI KUHUSU BABA AKE? SI ITAKUWA MARADUFU!!! HAIWEZEKANI HUYU MZEE “ X “ HAWEZI KUFURAHIA HESHIMA YA MTOTO WAKE WAKATI MIMI KILA SIKU NALIA NA UCHUNGU KWA USHENZI NINAO FANYIWA NA WANGU WA KUWAZAA MWENYEWE !!! LAZIMA NIMROGE HUYU KIJANA NA LAZIMA NIMRIPOTI KWENYE KIKAO!!!!
Baada ya hapo Mzee “ Y"atakacho kifanya ni kwenda kumripoti kijana “ A “ kwa mkuu wa kilinge.( , VILINGE VYA WACHAWI HUWA VIPO KARIBU KATIKA KILA SEHEMU NA MARA NYINGI HUWA VINAKUWA KWENYE MITI MIKUBWA NA HUWA VINAKUWA MAJINAAMBAYO MARA NYINGI HUBEBA MAJINA YA MAENEO. MFANO “ Mbuyuni”, “Mwembeni” “Mkuyuni”” Mwembe ….” Nakadhalika.
Kitakacho tokea baada ya wiki au miezi kadhaa wazazi wa kijana “ A “ wataanza kumuona kijana wao amebadilika kitabia katika namna ambayo hawakuitegemea wala kuitarajia.
Kijana msomi wa chuo kikuu utamsikia anazungumza maneno ya ovyo kama vile “ Oyaa Bi. Mkubwaa“, au “ Mshua unazingua !!“ na maneno mengine kama hayo pamoja na kufanya vitendo vya kilofa kama kuvalia suruali chini ya makalio, kunyoa viduku, kunywa viroba,kushinda bar anapiga story na wahuni na mwisho wa siku hayo ndio yanakuwa maisha yake .
Washirikina na wachawi huwa wanaishi maisha ya hovyo sana sema tu huwa wanajikaza mambo yao yasijulikane. Ubaya wanao wafanyia watu wengine huwa unawarudiaga wao wenyewe saba mara sabini hata baada ya miaka mingi.
Mchawi anapokufanyia ubaya huwa ni kama anajiwekea mwenyewe akiba ya ubaya ambao utakuja kumtokea baadae kabla ya muda wake wa kuishi haujamalizika hapa duniani. Kwa hiyo usishangae mzee Y anapo kasirika kusalimiwa kwa heshima na adabu na kijana A .
Katika uhalisia hayo ndio maisha ya wachawi katika levo ya familia. Kuna kisa kimoja kilitokea mwishoni mwa miaka ya themanini katika tarafa hiyo hiyo niliyo itaja hapo juu. Alihamia mtendaji mpya wa mtaa kutoka mkoa mwingine, baada ya kama wiki mbili hivi ikaletwa kesi ofisini kwake,. Kuna mzee mmoja gwiji amepigwa kwa mabapa ya mapanga na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe alieitwa Kulwa . Mzee alishachukua PF3 tayari na kwenda kutibiwa polisi, jalada lilishafunguliwa kituoni na huyo Kulwa yupo ndani . Sasa mzee gwiji ameingiwa na huruma ya uzazi anataka kwenda kumdhamini mahakamani mtoto wake japo yeye ndio muhanga wa tukio la uhalifu lililo fanywa na mwanae. Kwa kuwa mzee alikuwa anajisikia vibaya hawezi kwenda ofisini kwa mtendaji kuchukua karatasi ya dhamana, akamtuma shemeji yake, yaani mdogo wa kiume wa mke wake.
Shemeji mtu alipofika kwa mtendaji na kumsimulia kilicho tokea, mtendaji alisikitishwa sana.. “ Alihoji inakuwaje mtoto unampiga kwa mapanga baba ako mzazi! Dunia imekwisha “ . Wakati mtendaji ana saini karatasi za dhamana, akawa ana mdadisi yule shemeji mtu “ Imekuwaje kuwaje mpaka huyo kijana akampiga mapanga baba ake mzazi ?”.. Shemeji mtu akajibu “ Bwana we mambo ya kifamilia ndugu yangu !|. Mtendaji akasema “ Mambo ya kifamilia?!! Yani mambo ya kifamilia ndio mtu ampige mapanga baba ake mzazi ?!! DU sijawahi kusikia hiyo ndio naisikia mara ya kwanza”. “ Ila vyovyote vile, tuchukulie kwamba kweli huyo kijana aliudhiwa na baba ake kiasi cha kuamua kumshambulia kama njia ya kumaliza hasira zake. Kwanini basi asinge mpiga u hata ngumi, kwa sababu hayo mapanga si angeweza kumuua kabisa!! Na angemuua tungekuwa tunaongea habari nyingine tena “
Shemeji mtu akajibu “ Kulwa ampige ngumi baba ake ? Kulwa hanaga muda wa kurusha ngumi kumpiga baba ake. Kulwa yeye huwa anampigaga na mapanga tu au silaha yoyote ile itakayo kuwa karibu nae. Mwenye muda wa kurusha ngumi ni dotto. Dotto ndio huwa anampigaga ngumi baba ake. Aaaaaah huwa anampiga sana tena sana. Na kizuri baba mtu mwenyewe analitambua hilo. “ Shemeji mtu akaendelea kusema “ Lakini hata hivyo pamoja na kwamba Dotto huwa anampiga baba ngumi baba ake mzazi lakini huwa zinakuwa ngumi kali kweli kweli, unajua Dotto ni mtu wa mazoezi sana na ana maguvu sana. Mtoto kidogo mwenye afadhali ni kaka yao mkubwa na kina Dotto yeye huwa anamtia bakora tu baba yao. Yeye hanaga muda wa kushika silaha wala kumpiga ngumi, yeye huwa ni bakora tu. Na baba mtu anajua, kaka yao mkubwa akiwepo kama kuna sehemu ya kuchuma fimbo karibu , huwa hafanyi kabisa ujinga ujinga, kwa sababu anajua kijana wake atamtandika na bakora “
Mtendaji akataka kujua sababu inayo wafanya vijana hao wawe wanamkosea baba yao mzazi kwa kumpiga. Shemeji mtu akajibu, huyu mzee huwa anampigaga sana mama yao akitoka kwenye ulevi halafu akiwaga na hela huwa anaenda kuzimalizia kwa michepuko huko. Sasa vijana huwa wakisikia mama yao kapigwa au katukanwa, na wao huwa wanampiga baba yao. Wakimkuta na mchepuko pia huwa wanampa kisago baba yao.
Yule mtendaji alilewa na kubaki kusema “ Du ! Yani huyu mzee watoto wake wote huwa wanampiga . Dunia imekwisha “
Hao Kulwa na Dotto wakati wanafanya ujinga huo wa kumpiga baba yao walikuwa na miaka 37 na kaka yao alikuwa na miaka 40.
Katika mzingira kama hayo mzee kama huyu ambae watoto wake wa kuzaa mwenyewe wanampiga ngumi, mapanga na fimbo, hawezi kufurahishwa na heshima au adabau kutoka kwa kijana mtoto wa jirani yake . Huwa wanaumia sana.
Ndio maana miaka ya nyuma, vijana walishauriwa na kuambiwa kama hawana kinga ya wachawi wasi jipendekeze kabisa kwa wachawi kama alivyo fanya kijana A. Kuliko kujipendekeza ni bora wakae nao mbali kabisa. Kuliko kuonyesha wao ni vijana wenye adabu, bora wajifanye kujitoa akili pindi wanapo kutana na wazee wa aina hii hususani katika maeneo kama vile misibani nakadhalika. Huambiwi uwatukane, hapana, wewe kaa kimya na kama utalazimika kuzungumza basi zungumza mambo yanayo onyesha una maisha magumu, huna matumaini na umeharibikiwa kimaisha. Unatumia hiyo kama njia ya kuwapumbaza watu wabaya.
Jambo lingine ambalo ni la kawaida sana katika ulimwengu wa nyama lakini lina maana mbaya sana kwenye kamusi ya wachawi ni “ Sauti ya mtoto mchanga akilia “. Hakuna jambo lenye maana mbaya katika ulimwengu wa wachawi kama kusikika sauti ya mtoto mchanga akilia,na mbaya zaidi sauti hiyo itokekwenye nyumba ya eidha watu wa swala au ibada au ambao wamefunga ndoa halali.
Hakuna jambo linalo wakera kama kusikia sauti ya mtoto mchanga akilia kutoka katika familia ambayo mke na mume wameoana kwa ndoa rasmi.
Nirudi tena kwa kijana wetu.
Kijana huyu alianza kuwapigia wazee hao stori kama vile “ Nimepata kiwanja sehemu Fulani “. “ Nimeanza kufyatua matofali “ mara aanze kuwaambia “ Nimetoka kumpeleka fundi saiti kwangu “ au “ kesho nitaenda mjini kuchukua mabati, mbao “ na hadithi zinazo fanana na hizo.
Kijana huyu alikuwa anawaeleza wazee hao mipango yake kwa nia njema kabisa.
Aliwachukulia kama wazazi wake na alikuwa akiwaambia hivyo ili labda wampe ushauri wa kufuata hususani katika suala zima la “ ulinzi wa kiroho “
Ambacho hakukijua kijana huyo ni kwamba, sentensi alizo kuwa anazitamka kwa wazee hao, zilikuwa na maana mbaya sana katika kamusi ya uchawi.
“ Sisi tunaishi kwenye nyumba za udongo. Si watoto wetu wala wajukuu zetu ambao wamewahi kuwa na nyumba zao wenyewe achilia mbali nyumba ya kisasa kama anayo taka kuijenga kijana huyu.. Haya ni matusi makubwa sana kwetu.Hatuwezi kukubaliana na upumbavu kama huu!!! “
Wazee walicho kifanya wakaamua kumtia nuksi kijana huyo. Kwanza akafukuzwa kazi. Akashindwa kulipa mkopo benki, nyumba yake aliyokuwa anaijenga ambayo ndio kwanza ilikuwa imefikia kwenye lenta,ikapigwa mnada ( NYUMBA NYINGI KATIKA TARAFA HIYO HUWA ZINAISHIA KWENYE LENTA HUKU WAMILIKI WAKISALIA KUWA WALEVI WAKUPINDUKIA ).
Biashara yake ikafa. Akaingia kwenye ulevi wa pombe ulio pindukia.
Hapa kwenye ulevi wa pombe walimuacha kwa sababu alikuwa bado ana vihela hela, hivyo walimuacha ili hela alizo kuwa amebaki nazo azimalizie kwenye ulevi abaki hana kitu kabisa. Na kweli baada ya muda mfupi akawa ameishiwa hela. Kichwani mawazo, kazi hakuna, biashara imekufa, aibu mtaani, maneno yameanza kuzungumzwa.
Jamaa akaamua kuingia kwenye ulevi wa gongo ili aweze kusahau matatizo yake. Baada ya kama mwezi mmoja hivi jamaa akawa mlevi wa kupindukia anashinda kwenye vilabu vya gongo. Akawa anaonekana hajali tena kama aliwahi kuwa na kazi, biashara na maisha mazuri.
Wale magwiji hawakupendezwa na hali hii,kwa sababu wao walitaka kijana huyo baada ya kutiwa nuksi hiyo auone uchungu wa kuishimaisha ya kilofa na umasikini ulio tukuka na kibaya zaidi wakamfunga asiondoke kijijini hapo ili wawe wanamuona anavyo adhirika.
Taarifa za ulevi wa gongo wa kijana huyo hazikuwafurahisha hata kidogo,.Kwa sababu zilikuwa na maana mbaya sana katika kamusi yao.
Walicho kifanya wazee hao wakamtafuta kijana huyo na kumpa
dawa ya kuacha pombe..
Dawa hii ni tofauti na ile inayo changanywa na mayai ya ndege mmoja mweusi anaepaa au ile inayo changanywa na mavi ya ndege mmoja mweupe afugwae.
Hiidawa inatokana na mizizi ya mti mmoja wa porini wenye jina
linalo fanana na jina la wilaya moja iliyopo kusini mwa Tanzania. Huwa ni mwiko kwa mwanamke mjamzito kuuruka mzizi wa mti huu kwa sababu akifanya hivyo, mimba itaharibika.
Katika baadhi ya jamii za kiafrika, mtu anapokufa kwa kujiua mwenyewe,maiti yake huwa haingii ndani na kipande cha mzizi wa mti huu huwa kinachomekwa kwenye makalio ya mwili huo ili kuvunja roho ya kujiua katika m familia na ukoo huo.
Huwa unachukuliwa mzizi wa mti huo ambao umekufa wenyewe, kisha unasagwa halafu anapewa mlevi.
Kijana huyo alipopewa dawa hiyo alitapika sumu zote na toka
siku hiyo alichukia kabisa pombe na ulevi wa aina yoyote ile.
Kilicho fuatia baada ya hapo, kijana huyo akawa anafanya kazi
ambazo haziendani na elimu yake.
Kwanza akawa anabeba mizega ya maji, mara anazibua vyoo, mara anauzakaranga ilimradi watu wamuone anavyo adhirika. Wao hwafaidiki na chochote lakini wanafurahia kumuona kijana huyo akiwa anateseka na kudhalilika.
Kuhusu matumizi ya uchawi na ushirikina katika mchezo wa mpira wa miguu, Dokta Mungwa anasema,mambo hayo siku hizi hayafanyiki kama ilivyo kuwa inafanyika zamani. Siku hizi mambo yamebadilika tofauti na ilivyo kuwa zamani. Mambo yamebadilika sana siku hizi. Kwanza siku hizi vijana wanacheza mpira wa kulipwa tofauti na ilivyo kuwa zamani ambapo watu walikuwa wanacheza mpira wa ridhaa na kwa mapenzi ya timu husika.
Zama hizo watu walikuwa wanatumia sana uchawi katika mpira. Kila namba ilikuwa na uchawi wake na uchawi ulitofautiana kutoka timu moja na nyingine.
Kwa mfano, kwenye nafasi ya kipa
kipa ilikuwa kilikuwa kinachukuliwa kipande cha sanda iliyo tumika kumvesha maiti, kisha linachukuliwa karatasi jeupe ambalo yanaandikwa majina ya wachezaji wote wa timu pinzani kisha unawekwa unga wa kisiki ambacho watu wakipita njiani wanajikwaa kwaa na vitu vingine viwili ambavyo sita vitaja hapa. Baada ya hapo ilishonwa azima ambayo alipewa kipa na kutakiwa kuvaa kwenye mguu au mkono wowote.
Ndumba hii iliaminika kumsaidia kipa kuwa na uwezo mkubwa wa kudaka mipira awapo golini na pia kuwafanya wachezaji wa timu pinzani kuwa wanajikwaa kwaa na kuanguka wenyewe kila wanapo karibia lango.
Kwa wachezaji wanao cheza namba 2,3,4 na 5 ilichukuliwa mizizi ya nturantura kisha zinachongwa mpigi 4 ambazo kila moja itafungwa au kushonwa na nyuzi nyeusi kisha wanapewa wachezaji wa namba hizo na kuzivaa, baada ya kuzikaanga zote na majina ya wapinzani kwenye mafuta maalumu pamoja na dawa inaitwa Tunda la Jini au Tufahal Jinni. Dawa hizo zilimwagiwa kwenye kigae cha chungu kilicho vunjika wakati kikiwa kimebeba maji yaliyo chotwa kisimani. Baada ya hapo yaliandikwa majina ya wapinzani wote kwenye sahani maalumu nyeupe kwa kutumia zaafarani nyekundu na baadae kufutwa kwa kutumia vidole. Kila mchezaji alipewa mpigi 4 ambazo zilifungwa kwenye azima na kuzivaa.
Ama kwa upande wa viungo na washambuliaji, wao ilichukuliwa mizizi ya miti mitatu mkuyu, Mzungupori na Mtundaugoro,ambayo ilisagwa na kuchomwa pamoja hadi kuwa unga au majivu laini sana. Baada ya hapo ulichukuliwa upinde ambao ulitumika kuua nguruwe pori,upinde huo ulisagwa pia na kuchomwa hadi kuwa majivu,vyote hivi vilichanganywa na mafuta maalumu na kisha wachezaji hao walipakwa au kuchanjiwa.
Wakati mwingine ulitumika uchawi wa kuroga timu pinzani, kufanya wachezaji wote wa timu pinzani wakose pumzi wakiwa uwanjani, ambapo alikuwa anatumika mnyama mmoja na kamba maalumu.
Wakati mwingine mchezaji wa timu moja angeweza kufanya uchawi wakuwaroga wachezaji wenzake wanao gombania namba na kumfanya aonekane yeye ndio zaidi ya wenzake. Mfano mshambuliaji aliweza kufanyiwa uchawi, magoli yote afunge yeye mwenyewe au mafowadi wenzake wafunge kwa kupitia miguu yake. Fowadi huyu alinuiziwa kuwa goli lolote kutoka kwenye timu yake lisifungwe hadi lipitie kwanza kwenye mguu wake au kichwa chake.
Miaka hiyo ya zamani, uchawi na ushirikina kwenye mpira ulifanyika kama sehemu ya burudani ya mpira. Waganga walitumia michezo ya mpira wa miguu kushindanisha nguvu zao.
Wachezaji wali waogopa zaidi wachawi kutoka nje ya uwanja kuliko wachawi wa ndani ya uwanja.
Mchezaji wa mchangani alikuwa akipata nafasi ya kwenda kucheza kwenye timu kubwa basi ilifanywa siri hadi atakapo anza kuichezea rasmi timu hiyo kubwa.
Mwishoni mwa miaka ya themanini, kuna kijana mmoja katika kitongoji kimoja cha kwenye mkoa mmoja unaopatikana mashariki wa Tanzania alikuwa kiungo mshambuliaji hatari sana. Alikuwa anachezea timu mmoja iliyo kuwa inashiriki ligi daraja la tatu kipindi hicho. Basi mabosi wa timu moja kubwa wakamuona, wakawa wamemkubali sana, wakamfuata kuzungumza nae ili akasajiliwe kwenye timu hiyo kubwa, bila kuchelewa kijana akakubali na mipango ya kumchukua ikaanza kufanyika.
Alikuwa anatakiwa akaripoti klabuni siku ya Jumatatu kwa ajili ya kwenda kusaini mkataba mnono pamoja na kujiunga na wenzake kambini. Baba wa kijana huyo kwa furaha ya mtoto wake kusajiliwa kwenye timu kubwa akaanza kuwaambia, ndugiu, jamaa, majirani na marafiki. Habari zikawafikia magwiji na kama ilivyo tazamiwa,. Hazikuwapendeza. Magwiji wakaunda kamati ya kumuwekea zuio kijana huyo asiweze kwenda katika timu hiyo kubwa.
Ilikuwa siku ya Ijumaa, wazee wa mtaa wakamwambia baba wa kijana kuwa wameandaa sherehe maalumu ya kumuaga na kumpongeza kijana wao kwa sababu ameleta heshima kubwa sana kwenye mtaa wao. Kijana akatakiwa na yeye kuhudhuria. Baba mtu akakubali kwenda ili isionekane amekataa kwa sababu anaringa mtoto wake amesajiliwa kwenye timu kubwa. Kaka wa baba mtu ( Yani baba mkubwa wa kijana yule mchezaji ) nenda kwenye sherehe ila kijana asiende kwa sababu wanaweza kumlisha uchawi kwenye chakula atakacho kula. Baba mtu akasema “ Nisipoenda na huyu kijana itaonekana kijana amedharau wito wa wazee, ngoja niende nae tu, cha msingi sitaruhusu ale chakula kwenye sahani yake mwenyewe. Nitahakikisha chakula kinaletwa kwenye sahani ya kula watu wote kwa pamoja na ikiwezekana tule pamoja na wazee walio tualika “. Kaka mtu akamwambia “ WACHA UPUMBAVU BWANA MDOGO.. DAWA HUWA ZINANUIZIWA. MNAWEZA KULA WOTE CHAKULA KWENYE SAHANI MOJA LAKINI AKADHURIKA MTU MMOJA KWA SABABU ANAKUWA AMENUIZIWA MTU HUYO HUYO MMOJA, KWA HIYO CHA MSINGI HAPA .. KIJANA ASIENDE KABISA. WAAMBIE ANAUMWA NA KICHWA “
Baba wa kijana hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na ushauri wa kaka ake. Kijana kweli hakwenda kwenye hiyo sherehe kwa madai kwamba anajisikia kichwa kinamuuma. Mchana wa siku iliyo fuata sasa yani Jumamosi , kijana akaanza kulalamika kichwa kinamuuma, kichwa kinamchemka.
“ Baba kichwa kinauma, baba kichwa kinachemka !”. Inaelezwa kuwa joto la kijana huyo lilipanda kwa kasi ya ajabu katika namna ya kutatanisha. Inaelezwa zaidi kuwa kichwa cha kijana kilichemka kiasi kwamba ungeweza kuweka mtungi au sufuria la maji kichwani kichwani kwa kijana huyo yakachemka ndani ya muda mfupi kwa kiasi ambacho ungeweza kunyonyolea kuku !
Baba wa kijana hakuwa na jinsi zaidi kuwahisha kijana wake hospitali. Kufika hospitali madaktari kumpima wakakuta mtu alisha ondoka duniani toka enzi za Pontyo wa Pilato.
Nirudi kwa jamaa anaetaka Sanchez atupiwe uchawi wa kumfanya ashindwe kun'gaa kwenye timu yake mpya. Mawazo kama hayo yanaweza kukaa na kuishi ndani ya akili za wachawi tu. Hutakiwi kabisa kuwa na mawazo kama hayo.
Unamchukia mtu ambae hakujui wala hajui kama unamchukia na aathiriwi na chochote kuhusu chuki yako. Unadhani nani anae umia hapo kati yako wewe na Sanchez ?
Kumchukia mtu ambae hakujui wala hajui kama unamchukia, ni sawa na kuwapangisha kwenye nyumba yako, wapangaji ambao hawakujui na hawajui kama umewapangisha halafu wewe ndio unawalipa wao kodi. NI uwendawazimu.
Nafsi yako ni nyumba yako uliyo pewa na Mungu. Ndani ya nafsi yako unatakiwa uwapangishe wapangaji watakao kulipa kodi nzuri. Pangisha, furaha, amani, upendo, matumaini, imani nakadhalika. Ukipangisha chuki , husda na choyo, wewe ndio utakae umia. Utaishia kuvuna magonjwa kama presha, shinikizo la damu au kiharusi na kuvuta mapepo yatakayo endelea kukuletea nuksi kwenye maisha yako.
Kingine, unatakiwa kujua kuwa uchawi au uganga ni tofauti na mazingaombwe. Lazima uwe na sababu ya msingi na yenye akili. Hii ni kwa sababu uchawi ni gharama sana. Unahitaji vitu vingi ili jambo lililo kusudiwa liweze kutokea.
Ndio maana basi hata wachawi wenyewe wanapo taka kumroga mtu huwa wanaanza na njia za kawaida kwanza ambazo hazihusishi uchawi zikishindwa ndio wanaingia vitani rasmi kwa kuhusisha uchawi.
Kwa mfano wachawi wanataka kuwatenganisha mke na mume au mtu na mchumba wake. Kwa kuanza wataanza na umbea kwanza. Wanachukua maneno kwa mwanamke wanapeleka kwa mwanaume, wanachukua maneno kwa mwanaume wanapeleka kwa mwanamke. Wakiona mpango wao umeshindikana, hapo ndio wanatumia uchawi.
Ndio maana miaka ya nyuma watu walio kuwa wanaenda kwa waganga kutafuta suluhisho kwa mambo ya kipuuzi walikuwa wanaishia “kulaaniwa wao wenyewe “ na waganga hao.
Kwa mfano kulikuwa na baadhi ya wanaume, anaenda kwa mganga na kusema “ MGANGA NAOMBA UNIFANYIE DAWA ILI MKE WANGU ASIWE ANANIOMBA HELA YA MATUMIZI. ASAHAU KABISA KUHUSU KUNIOMBA HELA YA MATUMIZI HADI SIKU ANAINGIA KABURINI “
Mwanaume kama huyu ni mwanaume asie faa, kwa lugha nyingine anaweza kuitwa “ Khanithi “ . Mwanume wa hivi, kwanza alikuwa analazwa dhakari yake kwa kutumia akili yake ambayo imelala, halafu anafungwa kuzaa kabisa ili asirithishe upumbavu wake kwa watoto atakao wazaa... Na mwisho wa siku alitupiwa uchawi unaitwa “ SUNKHWA “ ama “ FUKUZA “ ambao ungemfanya aondoke kabisa kijijini hapo na kwenda kulowea kusiko julikana. Baadae lingefanyika tambiko maalumu la kutakasa kijiji hicho dhidi ya najisi ya mwanaume huyo.
Nimetoa maelezo haya ili kuwasaidia pia baadhi ya mashabiki wa Arsenal ambao wanaweza kuwa wameumizwa na kuondoka kwa Sanchez na ambao pia wanaweza kuwa na mawazo kama ya jamaa aliye taka nimroge Sanchez ili asipate mafanikio kwenye timu yake mpya.
Kama upo kwenye kundi hilo, huu ni ushauri wangu kwako :
1. JIPE MUDA UTASAHAU : Hakuna dawa nzuri ya kusahahu kitu au jambo unalo lipenda kama MUDA. Mwanzoni unaweza kuumia kumuona Sanchez akishangilia baada ya kuifungia timu yake mpya magoli kwenye mechi mbalimbali. Baada ya muda utazoea na utaona kawaida kabisa.
2. USIANGALIE MECHI ZA MAN U : Usiangalie mechi za Man U. Wewe subiri tu kuambiwa matokeo.
3. JITENGE : Siku ambayo Arsenal watacheza na Man U usitazame mpira pamoja na jamaa zako ambao ni mashabiki wa Man U. Nenda kaangalie mpira sehemu ambayo haujulikani.
4. HAMA MTAA UNAOISHI : Kama unadhani hauwezi kuwakwepa jamaa zako mashabiki wa Man U ambao watakua wanakuja kukukera wakishangilia namna Sanchez anavyo funga magoli, hama kabisa mtaa unaoishi/
5. BADILISHA NAMBA ZAKO ZA SIMU : Kwa sababu jamaa zako watakuwa wanakukera kukupigia simu kukwaambia kuhusu namna Sanhez anavyo fanya vitu vyake. Badilisha namba zako za simu ili wasikutafute kabisa.
6. BADILISHA OFISI AU ACHA KAZI KABISA : Kwa sababu si unasema wafanyakazi wenzako ofisini watakuwa wanakukera na habari za Sanchez. Basi kama ni mfanyabiashara, tafuta eneo jipya la biashara, au kama una ofisi yako, tafuta ofisi mpya au kama umeajiriwa, basi kazi kabisa ili uwe mbali nao.
7. HAMIA MAN U : Kwa sababu unampenda na unamkubali sana Sanchez na Sanchez ndo hivyo tena amehamia Man U. Kitu cha kufanya hapo wewe hamia Man U ili ukaendelee kuburudishwa na uchezaji wake.
8. JIFANYE HUJUI KAMA SANCHEZ ALIWAHI KUCHEZEA MAN U
9. FANYIWA TAMBIKO MAALUMU LA KUSAHAU KUHUSU SANCHEZ : Badala ya kuomba Sanchez asahau magoli, wewe ndio ufanyiwe tambiko maalumu la kusahau kuhusu Sanchez. Ukimuona Sanchez umuone kama takataka vile. Usikumbuke kama aliwahi kuchezea Arsenal.
10. 8. Kama unaona ushauri huo hapo juu ni UPUMBAVU basi kumchukia Sanchez kwa sababu kahamia MAN U pia ni UPUMBAVU ZAIDI.
Kitu kingine unacho takiwa kufahamu ni kwamba, Sanchez anatafuta maisha yake. Man U wamempa ofa ya kumlipa Pauni 500,000/= kwa wiki ambacho ni kiasi kikubwa sana cha pesa. Ni mpumbavu tu ndio anae weza kukataa ofa nzuri kama hiyo. HAKUNA MTU ASIEPENDA PESA. HATA WAZAZI WENU WANAWEZA KUWA WANAWAPENDA SAWA SAWA WAKATI MKIWA WATOTO WADOGO. LAKINI PINDI MTAKAPO ANZA KUJITEGEMEA WATAMPENDA NA KUMBARIKI ZAIDI MTOTO WAO ANAEWAJALI NA KUWATUNZA KWA KUWAPA PESA KULIKO WEWE AMBAE PESA ZAKO UNATUMIA KUFANYA STAREHE NA HUPELEKI MATUNZO KWA WAZAZI WAKO.
Imesimuliwa na DOKTA. MUNGWA KABILI....0744 000 473.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment