Shaka Ampiga Vijembe Maalim Seif

Wakati wananchi wa Jimbo la Kinondoni wakijiandaa na kampeni za ubunge wa jimbo hilo, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad akijiandaa kushiriki kampeni hizo kwanza awathibitishie wanachama wake ni lini ataapishwa kuwa Rais wa Zanzibar kama alivyowaahidi.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka amesema hayo jijini Dar es Salaam jana, mara baada ya kikao na watendaji wa sekretarieti za Wilaya za Dar es Saalam.

Shaka amesema Maalim Seif ni miongoni mwa wanasiasa ambao hawapaswi kusikilizwa na wananchi kutokana na kufanya siasa ionekane ni sehemu ya uongo kwani haaminiki.

“Maalim Seif kwanza awaambie wale aliowadanganya lini ataapishwa kuwa Rais wa Zanzibar, amewaongopea sana wanachama wake na sasa amechusha, kelele za kulilia urais wa Zanzibar kwa njia ya uongo zimezimika, tunamsubiri kwa hamu aje Kinondoani vijana tumejipanga kushughulika naye,” amesema.


from MPEKUZI

Comments