Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limesema mitihani ya kuhitimu kidato cha sita itaanza Mei 7 hadi 24, 2018.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Necta Januari 26, 2018 inaonyesha somo la kwanza litakuwa ni masomo ya jumla ‘General Studies’ na somo la mwisho litakalofanyika Mei 24 litakuwa ni Baiolojia 3C (kwa vitendo).
Msemaji wa Necta, John Nchimbi amesema “lengo la kutoa ratiba ni kuwafanya wanafunzi na walimu wao kujiandaa kwa ajili ya mitihani yao.”
“Ratiba inawasaidia wao kuweza kufanya maandalizi lakini kuwaweka sawa kisaikolojia na kujua mitihani ipo, itakuwa lini hadi lini na muda gani,” ameongeza
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment