Msanii wa muziki wa bongo fleva Nandy ambae anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake wa 'kivuruge' amefunguka na kudai hakuna mtu yeyote atakaeweza kumuunganishia kwa wanaume wenye pesa (pedeshee) bali kama watamuitaji wataenda wenyewe kwake.
Nandy ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo tetesi za muda mrefu zinazodai kwamba msanii huyo amesababisha kuvunjika kwa kundi la 'LFLG' kutokana na aliyekuwa meneja wake ambae ni Petit Man kumkuwadia kwa 'vigogo' huku akifahamu tosha kwamba mrembo huyo anatoka kimapenzi na Bill Nas ambae pia alikuwa mmoja wa wasanii katika kundi hilo.
"Mimi mtu hawezi kunipeleka kwa mapedeshe kama kunifuata watanifuata wao wenyewe, hawezi mtu kunipeleka kwa mwanaume sijafikia hatua hiyo. Na sina mazoea na Petit ya kuunganishiana mizigo", alisema Nandy.
Kwa upande mwingine, Nandy amesema haoni umuhimu wa kuongelea mambo ambayo hayana msingi katika kipindi huku akisisitiza kwamba jambo la muhimu kwa sasa ni 'kivuruge' kushika namba moja Tanzania nzima pamoja na wimbo wao mpya na Aslay 'Subalkher'.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment